27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

NCHI UNAZOWEZA KUMUDU GHARAMA ZA MAISHA, ADA

Na Joseph Lino


WATU wengi hutamani kwenda kusoma vyuo vikuu vya nje ya nchi, lakini ukiangalia gharama za ada na maisha ya kila siku ni kubwa kupita kiasi. 


Kuna baadhi ya nchi vyuo vyake vina gharama kubwa ya ada na mahitaji ya kila siku, lakini pia kuna nchi ambayo vyuo vyake hutoza ada ndogo na gharama ya maisha ni ya kawaida ikilinganishwa na nchi kama Marekani, Uingereza na Australia.
Wiki hii tunaangalia nchi ambazo gharama ya vyuo vikuu ni ndogo, hii inamanisha ada pamoja na gharama za maisha ya kila siku.
Nchi hizi unaweza kusoma ukiwa na bajeti ndogo na kuweza kumudu maisha.

Norway
Norway ni miongoni mwa nchi zenye gharama ndogo za ada katika kusoma kwenye vyuo vikuu vya umma. 

Pia inajulikana kuwa na  maisha bora, uzuri wa mazingira ya asili, na hakuna ubaguzi. Sababu nyingine ya kusoma Norway ni upatikanaji wa masomo ya Kiingereza katika ngazi zote.
Kwa upande wa gharama za maisha unatahitaji kiasi cha Dola za Marekani 14,530 kwa mwaka. 

Taiwan
Katika Bara la Asia, Taiwan ni moja ya nchi zenye gharama nafuu za kusoma kwa wanafunzi kutoka nchi zingine. Kwa mfano; Chuo kikuu cha National Taiwan, ada kwa wanafunzi wa shahada ya kwanza inaanzia Dola za Marekani 3,180 kwa mwaka.
Kuna kozi zaidi ya 120 ambazo zinafundishwa kwa Kiingereza katika zaidi ya vyuo 40.
Pia gharama za maisha ni za kawaida na kiwango cha chini  kwa gharama ya nyumba ni Dola za Marekani 2,330 kwa mwaka.

Germany
Ujerumani inajulikana kama nchi ya mawazo (the land of ideas), nchi hii inaendelea kuwa maarufu kwa wanafunzi wa kimataifa, kwa sababu ya vyuo bora na gharama ya chini maisha lakini pia maisha bora ya juu.
Hakuna ada ya masomo ambayo inatozwa katika ngazi ya shahada ya kwanza na shahada ya uzamivu katika vyuo vikuu vya umma.
Pia wanafunzi wa uzamili ambao hawajasoma shahada ya kwanza nchini Ujerumani wanalipa zaidi Dola za Marekani 10,800 kwa muhula, lakini unaweza kupata udhamini.

Kwenye gharama za maisha, utahitaji Dola za Marekani 9,500 hadi 10,480 kwa mwaka au zaidi lakini inategemea namna unavyoendesha maisha au matumizi yako. 

Ufaransa
Ada ya masomo katika vyuo vikuu vya Ufaransa hakuna tofauti ya ada kati wanafunzi wa nchi hiyo na wa kimataifa.

Lakini ada ni kubwa kwa baadhi ya vyuo ambavyo vina ada zao maalumu.
Aidha, gharama za maisha zipo juu katika mji mkuu wa Paris, lakini ni mji mzuri kwa wanafunzi  na umetajwa kuwa namba moja duniani kuwa mji wa wanafunzi kwa mara nne mfululizo.

Mexico
Mexico ni moja ya nchi za Amerika ya Kusini na kuna vyuo vikuu vingi ambavyo hutoa masomo kwa wanafunzi wa kimataifa.
Ada ya masomo hutofautiana ambapo vyuo binafsi hulipa zaidi, kwa wastani wa takribani Dola za Marekani 5,500 katika mji mkuu wa

Mexico City.
Gharama ya maisha ya kila siku ni ya kawaida nchini Mexico, mwanafunzi anaweza kutumia Dola za Marekani 500 kwa mwezi kwa bajeti ya Dola za Marekani 6,000 kwa mwaka.

India
India nayo ina vyuo vingi ambavyo gharama zake ni nafuu kwa ambao wanapenda kusoma huko. 
Lugha ya Kihindi ni maarufu kati ya lugha 100 za India, Kiingereza mara nyingi hutumika kama lugha ya kufundishia katika vyuo vikuu nchini humo hasa katika ngazi ya Uzamili.


Gharama za maisha ni nafuu, hata unaweza kutumia usafiri wa umma kwa Dola senti 25 kwa safari ya mora moja. 
Kwa upande wa ada ya masomo, hutofautiana kulingana na chuo na ngazi unayosoma, lakini kawaida si kubwa zaidi ya Dola za Marekani 7,300 kwa mwaka, na unaweza kuishi kwa raha kwa  Dola za Marekani 5,000 kwa mwaka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles