26.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 6, 2023

Contact us: [email protected]

KMC yaitishia Mbeya City

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

KITENDO cha kupata kuifunga Azam FC katika mchezo uliopita, kimeipa jeuri KMC FC baada ya kutamba kuendeleza ubabe kesho Novemba 27,2021 itakapoikabili Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya.

Mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakuwa was aba kwa KMC ambayo kati ya michezo sita imepata ushindi mechi moja ambayo waliifunga Azam mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, huku ikitoka sare miwili na ikipoteza mitatu.

Kwa upande wa Mbeya City haijapoteza mechi katika michezo sita iliyoshuka dimbani ikishinda miwili na sare nne na kukaa.

Mbeya City

Akizungumzia  maandalizi ya mchezo huo,  Kocha Msaidizi wa KMC, Habib Kondo, amesema  walijiandaa tangu Dar es Salama, Mbeya wamekwenda kupigania pointi tatu.

Ameeleza kuwa wanafahamu wanakutana na timu nzuri ambayo haijapoteza mchezo lakini anajua soka halichezwi kwa historia chochote kinaweza kutokea.

“Tuko na kikosi kamili, tumekuja kupambania pointi tatu, tumeshashinda mechi moja tunataka kushinda nyingine,” amesema Kondo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles