24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

MB Golden mwanamuziki anayewakilisha Afrika Mashariki Marekani

Na Mwandishi Wetu

MB golden ni Mtanzania anayeitangaza vizuri  Sanaa ya Tanzania  nchini Marekani kupitia muziki wa Bongo Fleva,  akiwa pia ni dansa na mfanyabiashara wa ubunifu anayemiliki  kampuni ya Massa Graphics.

Jina  lake halisi ni Mulette Ally, alizaliwa nchini Tanzania Desemba 02, 1997 na kukulia Nampula, Msumbiji kwa sasa ni mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Lebo ya SLR huku akijizolea umaarufu mkubwa kwa maelfu ya mashabiki katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Hadi sasa amekuwa msanii wa kwanza barani Afrika anayeishi Portland, Oregon Marekani kufikisha jumla ya watazamaji 100,000 kwenye mtandao wa YouTube.

Biashara na Muziki

MB Golden alianza kazi ya sanaa akiwa na umri wa miaka 16. mwaka 2012 alikuwa akiuza nguo na kukata nywele (kinyozi)  na pesa alizopata zilimuwezesha kurekodi wimbo wake wa kwanza unaoitwa na ‘Maisha’ alioshirikiana na R&B ambao  haukufanikiwa kibiashara.

Wimbo wake tishio ni Kibega ambao ulitolewa mwaka wa 2014 ambao  ulishinda tuzo tatu tofauti nchini Tanzania kisha akatoa studio albamu yake ya kwanza inayoitwa  “Bend Over” mwaka huo huo.

Tuzo

Mnamo 2015, MB GOlden alipata uteuzi wake wa kwanza katika tuzo za BCA 2015 za Msanii Bora Anayekuja ( Best Upcoming Artist).

Mafanikio Mengine

MB Golden ameendelea kufanikiwa kwa kuwekeza kwenye ubora wa kazi zake ndio maana amekuwa akishirikiana na  Sunday Alemeru ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni kubwa za uzalishaji picha na video nchini Marekani.

Video ya wimbo wa “Deamn Hot”, iliyoongozwa na Sunday Alemeru iliteuliwa kuwania tuzo ya Video Bora Afrika Mashariki 2021. Golden baada ya kusaini mkataba wa na lebo ya GVR Music mwaka 2019 alitoa studio albamu yake ya tatu ya ACTIA (2020).

Na mwaka 2021 umekuwa wa mafanikio kwake kwani alitoa wimbo mmoja unaoitwa Moto ambao umeendelea kutikisa chati za muziki Afrika Mashariki na Kati.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles