31.3 C
Dar es Salaam
Friday, December 2, 2022

Contact us: [email protected]

Klabu ya Rotary yatoa msaada wa madaftari 600 kwa wanafunzi wa Mbuyuni

Mwandishi Wetu

Wanachama wa Klabu ya Rotary ya jijini Dar es Salaam wamegawa madaftri 600 kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Mbuyuni iliyopo Oysterbay Ili kuwasaidia katika masomo yao.

Akizungumza baada ya kugawa msaada huo Rais mteule wa Klabu hiyo, Deborah Da Silva amesema wamemua kutoa msaada huo kwasababu elimu ndiyo msingi wa ukuaji wa uchumi.

Amesema Septemba ni mwezi wa elimu ya msingi na Kusoma na katika kusherehekea mwezi huu wanachama wa Klabu waliamua kukutana na wanafunzi kutoka shule hiyo kwasababu eneo hilo ni karibu na kitovu au ofisi Kuu ya klabu hiyo.

“Januari mwaka huu tulipata msaada kutoka Klabu ya Rotary ya Hereford ya nchini Uingereza, shule hii ilipewa pampu mpya kabisa ya kuchuja maji, tuliwapatia pia vitabu kwa ajili ya chumba kipya cha maktaba ambacho kilikuwa kinahitajika sana,” alisema Deborah.

Kwa upande wake Rais aliyemaliza muda wake, Farhat Lane alizungumzia elimu ya msingi ilivyo muhimu kwa ukuaji wa uchumi wa nchi ambapo alisema kujua kusoma na kuandika ni jambo muhimu kwa mafanikio ya mtu binafsi na ya jamii pia.

Alisema klabu za Rotary zina maeneo saba wanayoyalenga ambayo ni pamoja na elimu ya msingi na kusoma na kuandika, amani na kuzuia migogoro na utatuzi, kinga na tiba ya magonjwa, maji na usafi wa mazingira, afya ya mama na mtoto, maendeleo ya uchumi, jamii na mazingira. 

“Kwa kuzingatia hayo klabu yetu hufanya kazi kwa bidii kusaidia jamii zetu katika maeneo haya ya huduma na wanachama wa kilabu ambao wameundwa na wataalamu na marafiki wanaotaka kuleta mabadiliko Chanya katika jamii tunayoishi,” amesema Lane.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,507FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles