24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Kampuni ya Huawei yatoa mafunzo ya teknolojia ya 5G kwa watumishi wa umma

Mwandishi Wetu, Dodoma

Watumishi 24 na wahandisi kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (MWTC), Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Kampuni ya Mawasiliano Tanzania (TTCL Corp.) na Tume ya TEHAMA (ICTC) wametunukiwa vyeti vya kukamilisha mafunzo ya siku tisa ya teknolojia ya 5G.

Katika mafunzo hayo ya teknolojia ya 5G ambayo yametolewa na Kampuni ya Huawei Tanzania yamehusisha kundi la kwanza la wataalamu wa Kitanzania, ambao wamechukua kozi muhimu ya teknolojia za redio za 5G na upelekaji wa mtandao, mahitaji ya wigo wa 5G na upangiliaji, modeli za biashara za 5G na usimamizi wa 5G.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vyeti hivyo iliyofanyika jijini Dodoma, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dk Zainab Chaula, awapongeza wahitimu wa mafunzo hayo pamoja na Kampuni ya Huawei Tanzania akibainisha kuwa Serikali imedhamilia kuongeza uwekezaji kwenye nyanja ya dijitali.

“Tunahitaji kwenda na wakati na kujifunza maarifa na ujuzi wa kisasa ambao unakidhi mahitaji ya enzi hii ya dijitali na kuwa makini na mifumo ya kisasa ambayo inaweza kubadilisha au kuvuruga biashara na maisha yetu. Jambo la muhimu zaidi tunahitaji kuimarisha ustadi wetu kwenye TEHAMA kupitia mafunzo na uwezeshaji mpya ili kuendana na kasi ya mabadiliko, kukabiliana na changamoto na kuwahudumia watu wetu kwa ubunifu na ufanisi.”Alisema Dk Chaula.

 â€œUwekezaji huu umekuja wakati muafaka kwa kuwajengea uelewa wa kidigitali watumishi wa umma, na kwa kiwango kikubwa itasaidia uboreshaji wa jukwaa la huduma za kiserikali kidijitali, moja wapo ya vitu vitatu muhimu vya Programu ya Dijitali ya Tanzania, ni muhimu kwetu kukuza mazingira wazi na mfumo wa ikolojia ambapo kila mdau anaweza kushiriki, kuchangia, na kufaidika nayo, na ambayo itasababisha ukuaji endelevu wa sekta na maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini,’’ alisema

Akizungumza katika hafla hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Huawei Tanzania, Damon Zhang amesema tangu kuanza shughuli zake nchini mnamo mwaka 2007, Huawei Tanzania imejitolea kufundisha maarifa na ustadi wa TEHAMA kwa watanzania, na wataalamu wote kwa kuwajengea uwezo na utaalamu wa kimataifa huku akihamasisha vijana kuanza safari ya masomo yanayohusiana na TEHAMA.

“”Tangu tulipoanza shughuli nchini Tanzania mnamo 2007, Huawei Tanzania imejitolea kuhamisha maarifa na ustadi wa ICT kwa watanzania, na wataalamu wote kwa kuwajengea uwezo na utaalam wetu wa kimataifa na kuhamasisha vijana kuanza safari ya masomo yanayohusiana na TEHAMA.

“Tunafikiria kwamba nchini Tanzania watendaji wataweza zaidi kubuni maarifa ya kina yanayohusu TEHAMA na raia wa kawaida wataweza kuchunguza fursa na ustadi wa msingi kuhusu TEHAMA, na vijana ambao wanapenda masomo hayo wataijenga nchi kwenye misingi ya dijitali.”amesema Zhang

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles