23.3 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Klabu ya Rotary DSM Sunset yaadhimisha mwezi wa kuhamasisha elimu kwa kutoa msaada Mbuyuni

Katika kuadhimisha na kuhamasisha mwezi wa elimu, Wanachama wa Klabu ya Rotary Sunset ya jijini Dar es Salaam, wametoa msaada wa madaftri 600 kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Mbuyuni iliyopo Oysterbay jijini humo ili kuwasaidia katika masomo yao.

Akizungumza baada ya tukio la ugawaji wa madaftari hayo, Rais Mteule wa Klabu hiyo (PE), Deborah Da Silva amesema wameamua kutoa msaada huo kwa wanafunzi wa shule ya msingi kwa sababu ndiyo msingi wa elimu na ukuaji wa uchumi.

“Septemba ni mwezi wa elimu ya msingi na kusoma. Na katika kusherehekea mwezi huu, wanachama wa klabu tuliamua kukutana na wanafunzi kutoka Shule ya Msingi Mbuyuni kwa sababu eneo hilo ni karibu na kitovu au ofisi kuu ya klabu yetu.

“Shule ya Mbuyuni iko karibu na klabu yetu na ni katika shule hii ambapo klabu yetu ilizindua mradi wetu wa kwanza wa elimu mwaka 2019 ambapo tulifanya juhudi nyingi kutafuta fedha ili wanafunzi wapate maji safi ya kunywa.

“Januari mwaka huu tulipata msaada wa kutoka Klabu ya Rotary ya Hereford kutoka Uingereza, shule hii ilipewa pampu mpya kabisa ya kuchuja maji, tuliwapatia pia vitabu kwa ajili ya chumba kipya cha maktaba ambacho kilikuwa kinahitajika sana,” amesema PE Deborah.

Kwa upande wake Rais anayemaliza muda wake, Farhat Lane amezungumzia elimu ya msingi ilivyo muhimu kwa ukuaji wa uchumi wa nchi ambapo amesema kujua kusoma na kuandika ni jambo muhimu kwa mafanikio ya mtu binafsi na ya jamii pia.

“Umri wa mwanzoni wa mtoto ni msingi wa ukuaji wa baadaye na msingi mzuri wa ujifunzaji wa maisha yote, maendeleo ya utambuzi na kijamii,” amesema Lane.

Aidha Lane amesema Klabu za Rotary zina maeneo saba wanayoyalenga ambayo ni pamoja na elimu ya msingi, kusoma na kuandika, amani, kuzuia migogoro na utatuzi, kinga na tiba ya magonjwa, maji na usafi wa mazingira, afya ya mama na mtoto, maendeleo ya uchumi na jamii na mazingira.

“Kwa kuzingatia hayo klabu yetu hufanya kazi kwa bidii kusaidia jamii zetu katika maeneo haya ya huduma na wanachama wa klabu ambao wameundwa na wataalamu na marafiki wanaotaka kuleta mabadiliko chanya katika jamii tunayoishi,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles