27.3 C
Dar es Salaam
Monday, December 4, 2023

Contact us: [email protected]

Khoja Shia wafanya matembezi kuomboleza kifo cha Imam Hussain

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Jumuiya ya Waislamu ya Khoja Shia Ithanasheri imefanya matembezi ya kuomboleza kifo cha mjukuu wa Mtume Muhammad, Imam Hussain aliyeuawa miaka 1,300 iliyopita katika Mji wa Karbala Iraq.

Katibu wa Jumuiya ya Khoja Shia Dar es Salaam, Imran Sherali, amesema siku hiyo ya Ashura huadhimishwa kila mwaka kwa lengo la kumuenzi mjukuu huyo kutokana na matendo mema aliyoyafanya.

“Imam Hussain (a.s) alisimamia, kuamrisha mema na kukataza mabaya, matembezi haya leo katika ardhi ya Tanzania ni kwa sababu ya ujumbe wa amani aliokuwa amebeba Imam Hussain (as),” amesema Sherali.

Amesema Imam Hussain alileta umoja kwa binadamu wote bila kubagua dini wala rangi zao.

“Leo hii dunia inahitaji amani, amani imesambaratika, upendo umesambaratika. Lengo la matembezi haya kwa ajili ya Imam Hussain (as) ni kutaka kupaza sauti kwamba amani, utulivu na upendo ni moja ya mambo muhimu ambayo yanapaswa kuenziwa na kuangaliwa kwa makini,” amesema.

Jumuiya hiyo ya Khoja Shia Ithanasheri pia imekuwa ikitoa misaada ya kibinadamu huku pia ikimiliki hospitali ya Ebrahim Haji inayotoa huduma kwa gharama nafuu.

Hivi karibuni pia ilifungua kituo cha macho kilichopo Temeke kinachotoa huduma za macho bure pamoja na kufanya operesheni ya mtoto wa jicho. Pia inashirikiana na Mpango wa Damu Salama kufanikisha zoezi la uchangiaji damu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles