31 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 3, 2023

Contact us: [email protected]

Wizi wa mafuta wadhibitiwa bandarini

Na Brighiter Masaki, Mtanzania Digital

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla, amekagua kifaa cha kisasa cha kubaini wizi na upotevu wa mafuta ghafi kutoka bomba kuu ambacho kitaanza kufanya kazi leo.

Akizungumza na waandishi  wa habari wakati wa  ziara  aliyofanya leo Agosto 20, bandarini jijini Dar es salaam, Makalla, amesema upatikanaji wa kifaa hicho ni kutokana na maelekezo aliyoyatoa baada ya wizi wa mafuta uliofanyika Kigamboni.

“Agizo nililolitoa kwa TPA baada ya kuunda kamati ya ufuatiliaji upotevu wa mafuta ambapo miongoni mwa mapendekezo ya kamati ilikuwa ni ununuzi wa kifaa cha kudhibiti wizi wa mafuta bandarini.

“Nawahakikishia wafanyabiashara wa mafuta kuwa serikali imejidhatiti kumaliza kabisa tatizo la upotevu wa mafuta na nawashukuru kuwaona hadi sasa kumekuwa na matokeo mazuri.

“Nawapongeza Mamlaka ya Bandari  kwa kutekeleza maagizo ya  kununua kifaa cha kubaini wote walio na watakaochepusha mafuta kutoka bomba kuu,” amesema Makalla.

Amesema hadi sasa vyombo vya ulinzi na usalama vimewakamata na kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wa wizi  huo wa mafuta.

Pia Makalla ametembelea  ujenzi wa barabara za kuingia na kutoka bandarini na upanuzi wa eneo la kushusha na kupakia Mizigo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles