22.2 C
Dar es Salaam
Sunday, May 5, 2024

Contact us: [email protected]

KHLOE, THOMPSON WAANDAA MAKAZI YA MTOTO WAO

LOS ANGELES, MAREKANI


MWANAMITINDO maarufu nchini Marekani ambaye ni mdogo wake Kim Kardashian, Khloe Kardashian na mpenzi wake, Tristan Thompson, wameonesha jeuri ya fedha kwa kununua nyumba yenye thamani ya bilioni 44 kwa ajili ya makazi ya mtoto wao.

Wawili hao ambao wameanza uhusiano wao tangu Desemba mwaka jana, wanatarajia mtoto wao wa kwanza, hivyo wameamua kununua nyumba kwa ajili ya kuishi na mtoto huyo.

Kabla ya kununua nyumba hiyo, walikuwa wanaishi pamoja kwenye nyumba ya kupanga ambapo walikuwa wanalipa dola 6000 kwa mwezi, ambazo ni zaidi ya Sh milioni 133 za Kitanzania.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Khloe, amethibitisha kununua nyumba hiyo jijini Los Angeles, huku akidai kuwa wanataka kumpokea mtoto wao wa kwanza.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles