25.5 C
Dar es Salaam
Monday, May 13, 2024

Contact us: [email protected]

SHAHIDI: BASI LA LUCKY VINCENT LIMEWAHI KUMILIKIWA NA WATU WATATU

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mkoa wa Arusha, Nuru Suleiman ameieleza mahakama kuwa basi lililosafarisha wanafunzi wa Shule ya Lucky Vincent, lilikuwa linamilikiwa na mtu mwingine na si Mkurugenzi wa shule hiyo.

Amedai basi hilo limewahi kumilikiwa na watu watatu tofauti na mmiliki wa mwisho alikuwa Swalehe Kiluvia kabla ya Kampuni ya Lucky Vincent.

Suleiman ambaye ni shahidi wa pili katika kesi ya makosa ya usalama barabarani ikiwamo kusafirisha watoto bila vibali muhimu inayomkabili Mkurugenzi wa Shule ya Lucky Vincent, Innocent Moshi,

Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Arumeru, Desderi Kamugisha, amedai mahakamani hapo leo kuwa gari hilo pia halikuwa na leseni ya kubeba wanafunzi na badala yake lilikuwa na leseni ya kusafirisha abiria kutoka Arusha hadi Mererani.

“Baada ya kupokea barua kutoka kwa mpelelezi wa shauri linalohusu ajali hiyo ikinitaka kupata baadhi ya uthibitisho kutoka mamlaka tofauti kwa ajili ya upelelezi ambapo tuliandika barua Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), Idara ya Kazi, Mamlaka ya Mapato (TRA) na Kampuni ya Bima, Zanzibar Insurance,” amedai.

Shahidi huyo amedai barua hizo aliandika Mei 8, mwaka huu kwa taasisi hizo ili kufahamu kuhusu uhalali wa bima ya gari hilo, uchunguzi wa leseni ya usafirishaji, mkataba kati ya dereva na mmiliki wa gari pamoja na kutaka kujua iwapo gari hilo limewahi kumilikiwa na mtu mwingine.

“Mei 9, mwaka huu tulipata majibu kutoka taasisi hizo ambapo Sumatra ikieleza basi hilo halikuwa na leseni ya kubeba wanafunzi na badala yake lilikuwa na leseni ya kusafirisha abiria kutoka Arusha kupitia Mbuguni kuelekea Mererani, huku likionyesha mmiliki alikuwa ni mwingine anayetambulika kwa jina la Swalehe Kiluvia.

“Zanzibar Insurance walisema bima ya mwisho kukatiwa basi hilo ilikatwa na Kiluvia na Lucky Vincent hawakukata, hivyo kuendelea kutumia bima ya mmiliki mwingine, bima hiyo inakuwa siyo halali, huku Idara ya kazi ikitoa majibu kuwa ofisi hiyo haikuwa na mkataba wanaoutambua kati ya dereva wa basi hilo Dismas na shule hiyo,” amedai.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles