22.7 C
Dar es Salaam
Friday, August 12, 2022

Kevin Hart aonekana kwa mashabiki

LOS ANGELES, MAREKANI

STAA wa vichekesho na filamu nchini Marekani, Kevin Hart, juzi alionekana kwa mara ya kwanza mbele za watu katika tuzo za People Choice Awards baada ya kupata ajali mbaya ya gari Septemba mwaka huu.

Msanii huyo alipanda kwenye jukwaa hilo kwa ajili ya kutoa tuzo ya mchekeshaji bora wa mwaka kwa Robert Downey Jr, hivyo wakati wanapanda kwenye jukwaa hilo mashabiki walisimama na kumpigia makofi kwa kuwa ndio mara ya kwanza wanamuona.

Hata hivyo, kabla ya kutoa tuzo hiyo, Hart alianza kwa kumshukuru Mungu kwa kumfanya kuwa hai pamoja na kuwashukuru mashabiki kwa maombi yao.

“Kitu cha kwanza na muhimu ni kumshukuru Mungu, kwa kuwa bila ya yeye nisingeweza kuwa hapa, kutokana na hayo nishukuru kuendelea kuwaona mashabiki zangu, nitumie nafasi hii kumshukuru mke na watoto wangu, wana mchango mkubwa wa maisha yangu, niseme asanteni,” alisema msanii huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,580FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles