Dulla Makabila: Situmii mkorogo

0
1159

GLORY MLAY

MSANII maarufu wa singeli, Dulla Makabila, amekanusa madai ya kuwa anatumia mafuta ya kemikali ‘mkorogo’yanayomfanya kuwa mweupe.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Makabila alisema zamani rangi yake ya weupe ilififia kutokana na shida, kutokana na kipato anachopata rangi yake imerudi.

“Mimi sijichubui kama watu wanavyosema, nilizaliwa na rangi hii, lakini kutokana na shinda ambazo nilipitia hasa katika kufanya biashara kwenye jua ndizo zilinifanya rangi yangu ififie.

“Sasa namshukuru Mungu mambo yamebadilika riziki napata na rangi yangu imerudi, sijawahi kutumia vidonge au mkorogo wa aina yoyote ili niwe hivi” alisema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here