22.2 C
Dar es Salaam
Saturday, October 1, 2022

KCB YADHAMINI LIGI KUU TANZANIA BARA

 

Na ZAITUNI KIBWANA, DAR ES SALAAM


SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) na Benki ya KCB, wamesaini mkataba wa mwaka mmoja wenye thamani ya Sh milioni 420 kudhamini Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu wa 2018/19.

TFF wamefikia makubaliano hayo na KCB, baada Kampuni ya Vodacom ambao ndio waliokuwa wadhamini wakuu kumaliza mkataba.

Mkataba huo umesainiwa jana na Rais wa TFF, Wallece Karia na Mkurugenzi Mtendaji wa KCB, Cosmas Kimario, kwenye Hoteli ya Serena, Dar es Salaam.

Katika udhamini huo, klabu 20 kila mmoja itapata Sh milioni 15, ambapo fedha nyingine zitatumika katika shughuli mbalimbali za ligi kwa mujibu wa mkataba huo.

Akizungumza katika hafla hiyo, Karia aliishukuru benki hiyo na kusema kuwa bado wapo kwenye mazungumzo na benki hiyo ili kuona uwezekano wa benki hiyo kudhamini ligi nyingine kama daraja la kwanza, wanawake na nyinginezo.

“Tunawashukuru KCB ila lengo la TFF ni kupunguza makali kupitia wadhamini, ligi yetu ni ndefu na timu zinahitaji kuwa na fedha za kutosha,” alisema.

Alisema wanaendelea na mazungumzo na wadhamini wengine na wanaamini watafanikiwa kuanza ligi wakiwa na mdhamini mkuu.

Kwa upande wake, Kimario alisema benki yao ni wadau wakubwa wa maendeleo ya michezo nchini, hususani mpira wa miguu.

Alisema msimu uliopita walipata mafanikio makubwa katika udhamini huo na kuamua kuendelea msimu huu.

“Tumefarijika sana na udhamini wa msimu uliopita, ambapo kama mtakumbuka tulisaini mkataba wenye thamani ya Sh milioni 325, hivyo tumeona mafanikio makubwa,” alisema.

Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi (TPLB), Boniface Wambura, aliziomba klabu zinazoelekea kupata wadhamini kuwasilisha mikataba yao ili kuondoa ukinzani endapo TFF itapata mdhamini mkuu ambaye ni mshindani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,373FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles