24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

‘LIKIZO YA UZAZI KWA WANAUME SI YA KUNYWA POMBE’

 

|Veronica Romwald, Dar es Salaam



Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amewataka wanaume kutoitumia likizo ya siku tano ya uzazi kwa wanaume kwenda kunywa pombe.

Aidha, amesema ataifuta likizo hiyo kwa wanaume endapo atajiridhisha haina manufaa na inatumika ndivyo sivyo.

Akizungumza kuhusu Wiki ya Unyonyeshaji itakayoanza kesho hadi Agosti 8, mwaka huu, Waziri Ummy amesema likizo hiyo ni kwa ajili ya kumsaidia mama anapokuwa amejifungua na si vinginevyo.

“Likizo ya uzazi kwa wanaume si ya kwenda kunywa pombe, lakini wapo wanaume wanachukua likizo na nyumbani hawaonekani, nitafanya utafiti kuangalia iwapo ina manufaa kama hakuna tutaifuta,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles