29.7 C
Dar es Salaam
Wednesday, August 17, 2022

Katwila atamba kuendeleza makamuzi kwa KMC

 NA MOHAMED KASSARA-DAR ES SALAAM

KOCHA wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila ametamba kuwa watahakikisha wanaendeleza shangwe zao kwa kuichapa KMC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaochezwa leo kwenye Uwanja wa CCM Gairo, mkoani Morogoro.

Mtibwa Sugar itashuka dimbani kuikabili KMC ikitoka kushinda Kombe la Mapinduzi kwa kuifunga Simba bao 1-0 katika mchezo wa fainali uliochezwa Januari 13, mwaka huu, Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Katwila alisema watahakikisha wanaendeleza moto wao waliouwasha katika michuano ya Mapinduzi kwa kuichapa KMC ili kujiongezea pointi tatu muhimu.

Alisema kikosi chake kimepanga kushinda mchezo huo ili kuwapa raha ya ubingwa mashabiki wao wa Mji Mdogo wa Gairo ambao upo uwanja wanaotumia kwa sasa.

“Baada ya kumaliza michuano ya Mapinduzi tukiwa mabingwa, sasa tunarudi kwa kasi kwenye ligi. Tunaikabili KMC tukiwa mabingwa, hivyo morali ya wachezaji ipo juu mno na kila mmoja anataka kushinda mchezo huo ili kukoleza shangwe za ubingwa huu.

“Tunajua mechi za ligi ni tofauti na zile za Mapinduzi, lakini kuzifunga Simba na Yanga katika michuano hiyo kumetuongezea ari mpya, tunataka kushinda ili kuwapa zawadi mashabiki wetu wa Gairo, tunatambua mchango wao, hivyo hatutawaangusha,” alisema Katwila ambaye beki wa zamani wa timu hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,905FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles