DC Kinondoni apiga marufuku walimu wanaowakataa wanafunzi kidato cha kwanza

  0
  567

  Faraja Masinde, Dar es Salaam
  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo amepiga marufuku walimu wa Shule za Sekondari wilayani humo wanaoshindwa kuwapokea wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa kigezo cha kutotimiza mahitaji.
  Chongolo amepiga marufuku hiyo leo Ijumaa Januari 17, Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuwapongeza walimu wa shule za sekondari wa Wilaya hiyo baada ya kushika nafasi ya tatu kitaifa kwa ufaulu.
  “Nimarufuku kwa Mwalimu Mkuu kushindwa kumpokea mwanafunzi wa kidato cha kwanza kwa kigezo cha kutokuwa na sare au dawati kwa kuwa hivyo haviwezi kuwa sababu ya yeye kutokupokea anachofundishwa darasani,” amesema Chongolo.
  Awali, Meya wa Manispaa hiyo,Benjamini Sitta amesema kuwa licha ya wilaya hiyo kuongoza kwa asilimia 97.1 Lakini bado inakabiliwa na changamoto ya miundombinu ya elimu ikiwamo Madawati kwa kuwa kila mwaka kuna ongezeko la wanafunzi.

  “Manispaa yetu pamoja na kwamba tumefanya vyema lakini bado tunakabiliwa na changamoto ya miundombinu ya elimu ikiwamo madarasa na madawati.
  “Kila mwaka kuna ongezeko la asilimia 7 ya wanafunzi hivyo bado kuna kazi ya kufanya kwa Manispaa yetu ili kuhakikisha kuwa mwakani tunafikisha asilimia 100 ya ufauli,” amesema Sitta.
  Katika hafla hiyo ya kuwapongeza kila mwalimu ambaye amefaulisha kwa alama A ya kila somo atapata Sh 10,000.

  LEAVE A REPLY

  Please enter your comment!
  Please enter your name here