20.8 C
Dar es Salaam
Saturday, August 20, 2022

Mexime awamwagia sifa wachezaji wake

Na THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Mexime, amewamwagia sifa wachezaji wake kwa kutulia na kuibuka na ushindi katika mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Yanga, uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Katika mchezo huo, Kagera Sugar waliinyuka Yanga mabao 3-0.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Mexime alisema mpira ni dakika 90 hivyo yule aliyecheza juu ya mwenzake ndio ameibuka na ushindi.

“Nawapongeza wachezaji wangu kwa kuonyesha soka safi katika mchezo huu na kupata ushindi mnono, kwani tulitoka kupoteza michezo kadhaa huko nyuma, tusingekubali kupoteza kwa mara nyingine,” alisema.

Alisema licha ya kupata ushindi, hata wapinzani wao Yanga walikuwa vizuri lakini wao walitumia makosa waliyofanya na kupata ushindi. Mexime alisema ushindi huo umewapa nguvu ya kuendelea kufanya vizuri katika mechi nyingine zilizo mbele yao ili wapate ushindi na kujiweka katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
199,058FollowersFollow
551,000SubscribersSubscribe

Latest Articles