25.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 17, 2021

Kanye West atangaza kuwania urais wa Marekani

New York, MAREKANI

MWANAMUZIKI Maarufu nchini Marekani  Kanye West amesema anatarajia kuwania urais wa Marekani katika uchaguzi ujao.

Haifahamiki kama mwanamuziki huyo amemaanisha kweli kile alichokisema, au hiyo ni njia tu ya kutafuta kuzungumziwa tu ifahamikavyo na wengi (Kiki) limeeleza shirika la habari la Bloomberg.

West aliweka ujumbe kwenye mtandao wa Twitter siku ya Jumamosi usiku na kusambaa mitandaoni, huku ukirudiwa kuchapishwa mara 100,000 ndani ya kipindi cha saa nne.

West ana wafuasi milioni 29.4 kwenye mtandao wa Twitter ambao walisambaza kwa haraka akawa ndiye anayezungumziwa zaidi kwenye mtandao huo nchini Marekani.

“Lazima sasa tutambue ahadi ya Marekani kwa kumuamini Mungu, kuunganisha maono yetu na kujenga mustakabali wetu,” West aliandika akinukuliwa na gazeti la The Guardian.

Kama West alichokisema kilikuwa si cha masihara, basi kuna mlolongo mrefu wa vihunzi katika kuelekea azma hiyo, ikiwemo kuanza kampeni tangu awali mwezi Julai mwaka huu wa uchaguzi ikiwa imebaki miezi minne kabla ya kura za Novemba 3, mwaka huu.

Atahitaji kufuzu katika majimbo 50 na pia kujenga taasisi ya kisiasa kuanzia mwanzo bila usaidizi.

Kwa sasa, West hajaonekana kujaza fomu za tume ya uchaguzi nchini humo kwa ajili ya kuwania nafasi hiyo ya juu, kwa mujibu wa Bloomberg baada ya kupitia data za tume hiyo FEC,

West mwenye umri wa miaka 43, alizungumzia suala la kuwania urais miaka kadhaa nyuma, na mwaka jana aliiambia hadhira yake kuwa atawania urais mwaka 2024.

Yeye na mkewe, Kim Kardshian West, wamekuwa wakifanya kazi na rais Donald Trump mara kadhaa ikiwamo wakati wa shughuli za kuwafungulia wafungwa.

West na mkewe walishawahi kumtembelea Trump kujadili mabadiliko katika magereza mwaka 2018, baada ya mkutano huo West alimsifu Trump akisema amemfanya kujihisi shujaa, akamkumbatia na kukiri: ”Ninampenda huyu mtu.”

Trump alipoulizwa kama West anaweza kuwa rais siku moja , alijibu: ”Sana tu anaweza kuwa.”

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
156,567FollowersFollow
517,000SubscribersSubscribe

Latest Articles