Trump aapa kumshinda mpinzani wake

0
448

Washngton, MAREKANI

RAIS wa Marekani Donald Trump ameapa kuwashinda wapinzani wake katika uchaguzi mkuu utakaofanyika hivi karibuni.

Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya uhuru katika bustani ya Ikulu ya Marekani akiwa ameambatana na mke wake Melania, Trump alisema atawashinda wapinzani wake wa mrengo wa kushoto.

Alisema wapinzani wake wana mawazo ya Marxi, wanaopinga serikali na wenye nia ya kufitini na waporaji.

Trump ametoa majigambo hayo katika hotuba yake ya huku akiahidi kupigania maisha ya wamarekani.

 Trump aliwashutumu waandamanaji wa ‘Black Lives Matter’ waliokuwa wamekusanyika katika maeneo ya karibu kwa kuharibu masanamu ya wanaotajwa katika historia ya Marekani kupitia maandamano ambayo yamekuwa yakifanyika siku za hivi karibuni yanayopinga ubaguzi wa rangi.

“Lengo lao ni kuharibu tu,” alisema Trump

Akizungumzia ugonjwa Covid 19, Trump alisema kabla ya mwisho wa mwaka huu nchi hiyo itakuwa na tiba na au chanjo.

Alisema kuwa China ndio kitovu cha virusi vya corona hivyo inastahili kuwajibishwa kikamilifu.

 Alisema Marekani imepima takriban watu milioni 40, na kuongeza kuwa asilimia 99 ya maambukizi ya virusi vya corona havina madhara.

Marekani ina idadi kuwa ya waliokufa kwa virusi vya corona na kupata maambukizi na imethibitisha maambukizi mapya 43,000 ndani ya saa 24 Jumamosi, kulingana na takwimu za chuo kikuu cha Johns Hopkins, Florida, ambako hasa idadi ya walioambukizwa imeongezeka na kufikia maambukizi 11,458.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here