23 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 18, 2024

Contact us: [email protected]

Kampeni ya ‘NMB Kama Upepo’ yazinduliwa, washindi kupaa Dubai

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

BENKI ya NMB imezindua kampeni ya ‘NMB Kama Upepo,’ iliyotokana na Makubaliano ya Kibiashara na Kampuni ya Skylink Travel & Tours, inayojihusisha na uwakala wa tiketi za ndege, kampeni itakayowazawadia washindi sita na wenza wao safari iliyolipiwa gharama zote kwa siku tatu nchini Dubai.

Afisa Mkuu Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (wa pili kulia), akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya NMB Kama Upepo inayolenga kuchagiza matumizi ya kadi za NMB Mastercard na QR  kwa ajili ya kununua tiketi za ndege za Skylink. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Meneja Uendeshaji wa Skylink, Solomon Mwale, Mkurugenzi wa Skylink, Moustafa Khataw na Mkuu wa Idara ya Biashara za Kadi NMB, Philbert Casmir. (Na Mpiga Picha Wetu).

‘NMB Kama Upepo’ ni kampeni itakayoendeshwa kwa miezi mitano, ikilenga kuchagiza matumizi ya kadi za NMB MasterCard na QR Code miongoni mwa wateja wa benki hiyo kwa ajili ya kununua tiketi za ndege, ambako watapata punguzo la asilimia 60 ya ada ya huduma (service charges).

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ‘NMB Kama Upepo’, uliofanyika jijini Dar es Salaam (Jumanne Agosti 31), Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara, Filbert Mponzi, alisema kampeni hiyo itakuwa na zawadi za kila wiki na kila mwezi kwa wateja wa NMB watakaofanya malipo ya tiketi za ndege kutoka Skylink kwa kutumia MasterCard na  QR Code.

“Kadri mteja atakavyotumia kadi katika manunuzi ya mitandaoni au kufanya malipo kupitia kadi za NMB kwenye tovuti ya Skylink, ama mashine zetu za malipo (POS) zilizoko katika ofisi za washirika wetu hawa, ndivyo atavyojiongezea nafasi za kushinda zawadi kutoka kwetu

“Katika kipindi chote cha kampeni hii ya NMB Kama Upepo, inayoanza Septemba 1, 2021 hadi Januari 2022, washindi sita na wenza wao (jumla watu 12), tutawazawadia safari iliyolipiwa gharama zote, ikiwamo malazi kwa siku tatu huko Dubai, tiketi za ndege za kwenda huko na kurudi nchini, pamoja na pesa za matumizi,” alisema Mponzi.

Afisa Mkuu Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (wa pili kulia) na Mkurugenzi wa Skylink, Moustafa Khataw wakizindua kampeni ya NMB Kama Upepo inayolenga kuchagiza matumizi ya kadi za NMB Mastercard na QR code kwa ajili ya kununua tiketi za ndege za Skylink. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Meneja Uendeshaji wa Skylink, Solomon Mwale na kulia ni Mkuu wa Idara ya Biashara za Kadi NMB, Philbert Casmir. (Na Mpiga Picha Wetu).

Aidha, Mponzi alifafanua kuwa, NMB Kama Upepo ni kampeni chanya yenye lengo la kupunguza matumizi ya pesa taslimu na kwamba iko wazi kwa wateja wote wanaomiliki kadi za NMB MasterCard, sambamba na wale wote ambao wameomba ama watakaoomba kadi mpya wakati kampeni hiyo ikiendelea.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Skylink, Moustafa Khataw, alisema Skylink ina furaha kubwa sio tu kuingia makubaliano ya kibiashara na NMB, bali pia kuwa sehemu ya Kampeni ya NMB Kama Upepo, na kwamba wateja wa benki hiyo watafurahia huduma chanya zinazoenda kutolewa katika miezi yote ya uwepo wake.

“Tuna furaha kufanikisha makubaliano haya, yanayoenda sambamba na uzinduzi wa NMB Kama Upepo. Tunaishukuru Menejimenti ya NMB kwa ushirikiano huu na ahadi yetu kwa wateja wa benki hiyo Ni kuwahakikishia huduma bora, nafuu, salama na rahisi ya manunuzi ya tiketi,” alisema Khataw.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles