24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yataka fursa za kiuchumi Ziwa Viktoria zitangazwe

Na Clara Matimo, Mwanza

Serikali imetoa wito kwa Chemba ya Wafanyabiashara, Wenye  Viwanda na Kilimo (TCCIA) ambao ni waandaaji wa Maonesho ya Biashara  ya Afrika Mashariki kuweka sehemu za kutangaza fursa za kiuchumi zinazopatikana katika Ziwa Victoria mkoani Mwanza katika maonesho yajayo ya mwaka 2022.

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza, Amina Makilagi katikati akizindua  maonesho ya 16 ya Biashara Afrika Mashariki yanayofanyika uwanja wa Rock City Mall kwa niaba ya Mkuu wa mkoa huo, Mhandisi Robert Gabriel, kushoto kwake ni Mwenyekiti TCCIA Mkoa wa Mwanza, Gabriel Kenene, kushoto ni Kaimu Katibu Tawala mkoani humo emily Kasagala. Picha na Clara Matimo.

Wito huo umetolewa  jijini Mwanza Jumanne Agosti 31, 2021 na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi, alipokuwa akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel, kwenye ufunguzi wa maonesho ya 16 ya biashara Afrika Mashariki yanayoandaliwa na TCCIA Mkoa wa Mwanza kila mwaka ambapo mwaka huu yanafanyika katika uwanja wa Rock City Mall.

Amesema  fursa zilizopo ndani ya ziwa hilo zikitangazwa na wananchi wakazitumia ipasavyo zitawasaidia katika kukuza uchumi wao binafsi, mkoa na taifa kwa jumla.

“Sisi kama Serikali tayari tumeanzisha mradi ambao utatumia maji ya Ziwa Victoria tunauita blue economy, mradi huu utatoa fursa kwa makundi mbalimbali wakiwemo vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kushiriki katika  shughuli ya ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba.

“Wizara ya mifugo na uvuvi imekubali kutoa mafunzo kwa vikundi vyote vyenye nia ya kuwekeza katika ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba pia wizara hiyo imetoa ofa ya kufanya maping ili kuelewa maeneo yote yanayofaa kwa ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba, basda ya kubaini maeneo vikundi hivyo vianze shughuli ya ufugaji,” amesema Makilagi.

Naye Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza, Emil Kasagala, amesema  Tanzania inamiliki asilimia 53 ya maji ya ziwa victoria  kati ya hizo asilimia 49  yako katika mkoa huo na nia ya Serikali ni kuhakikisha wananchi wananufaika na rasilimali zilizopo katika maeneo yao ndiyo maana  imeanzisha mradi huo.

“Tumekwishachukua hatua mbalimbali katika kufanikisha mradi huu, tumepata wawekezaji ambao wako tayari kuwekeza kiwanda cha kutengeneza vizimba na vyakula vya samaki,” amesema Kasagala na kuongeza.

“Tunaendelea kufanya mazungumzo na taasisi tofauti tofauti za fedha  ili wawakopeshe watu watakaokuwa na nia ya kuwekeza katika ufugaji wa samaki  hivyo tumehamasisha  na tunaendelea kuhamasisha makundi mbalimbali yajiunge katika vikundi maana itakuwa rahisi kukopesheka,” amesema Kasagala.

Kasagala amewataka wananchi wa Mkoa wa Mwanza kuchangamkia fursa hiyo kwa kuwa  samaki  zinasoko la uhakika ndani na nje ya nchi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Mwanza, Gabriel Kenene, ameishauri Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuongeza kasi ya kutoa elimu  kwa wananchi kuhusu  ulipaji kodi.

“Watanzania wengi wana nia ya kulipa kodi lakini hawana elimu ya kutosha TCCIA tunaamini mkiwaelimisha vizuri watalipa kodi  na uchumi wa nchi yetu utapanda zaidi,” amesema Kenene

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles