25.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 28, 2024

Contact us: [email protected]

HESLB yaongeza muda mikopo ya wanafunzi

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imeongeza muda wa uombaji mikopo kwa siku 15, ikianzia  Septemba 1 -15, huku wale waliopo JKT  ni Septemba 20-30, ili kuwapa fursa waombaji mikopo ambao wamejisajili katika mfumo kukamilisha maombi yao.

Hayo yamezungumzwa na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdulrazack Badru mbele ya waandishi wa habari  na wawakilishi kutoka Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) na Shirika la Posta Tanzania (TPC) ambao pia wanawahudumia waombaji mkopo.

Badru amefafanua kuwa uamuzi huo umetokana na maombi na ushauri walioupokea kutoka kwa wadau.

“Tulianza kupokea maombi kwa njia ya mtandao Julai 9, mwaka huu, hadi jana ambayo ilikua siku ya mwisho ya kuomba tulikua na waombaji 91,445 waliowasilisha maombi, kati ya hayo, maombi 12,252 yalikua hayajakamilika na wateja wetu wameomba muda wa kukamilisha,” amesema Badru.

 Ameeleza kuwa hatua inayofuata ni uhakiki wa nyaraka na taarifa zilizowasilishwa na waombaji 79,193 ambao maombi yao yamekamilika kama yanavyoonekana katika  mfumo.

“Kuna makundi mawili, wale 12,252 ambao maombi hayana viambatisho na hivyo hayajakamilika na kuna maombi 79,193 yenye nyaraka, sasa tunaanza kuhakiki usahihi wake na baadae tutaangalia kama wamepata udahili na wale wenye sifa ndiyo watapangiwa mkopo,” amesema Badru.

“Tumekuwa tukiwasiliana na Makao Makuu ya JKT, na tumekwenda na kukutana na vijana hao katika kambi zote na tuliwaahidi kuwa watapata fursa ambayo ni kuanzia Septemba 20 hadi 30 mwaka huu, hivyo wasiwe na wasiwasi,” amesema Badru.

Ametaja bajeti ya mikopo kwa mwaka wa masomo wa 2021/2022 Serikali imetenga kiasi cha sh. 570 bilioni kwa ajili ya kugharamia mikopo ya wanafunzi 160,000 wa taasisi za elimu ya juu.

“Kati ya hao, wanafunzi 62,000 wanatarajiwa kuwa ni wa mwaka wa kwanza na wanafunzi 98,000 wanaoendelea na masomo. Bajeti kwa mwaka 2020/2021 ilikua sh. 464 bilioni na zimewanufaisha jumla ya wanafunzi 149,398,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles