24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Wahandisi 630 kula kiapo

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

JUMLA ya wahandishi 630, wanatarajia kula kiapo cha utii wa taaluma yao ili kuhakikisha kuwa wanawajibika vyema katika maamuzi pamoja na utendaji wa kihandisi ambapo kiapo hicho kitatumiwa na vyombo mbalimbali kuwawajibisha watakapo kiuka sheria na taratibu katika majukumu yao.

Hayo yameelezwa na  mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkutano mkuu wa Bodi ya Usajili Wahandisi nchini (ERB) Prof, Bakari Mwinyiwiwa, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya siku ya Wahandisi Tanzania mwaka 2021.

Prof.Mwinyiwiwa amesema  maadhimisho hayo yamepangwa kufanyika jijini Dodoma, kwa siku mbili, kesho Alhamisi  na keshokutwa katika ukumbi wa Jakaya Kikwete.

Amesema  kuwa kiapo kitaufanya umma ujenge imani kwa Wahandisi husika na kitatumika dhidi ya mhandisi atakapo vunja miiko na maadili ya taaluma katika kumchukulia hatua Mhandisi atake kiuka kiapo chake.

“Kiapo kitamlinda mhandisi dhidi ya kulazimishwa kutenda mambo ambayo ni kinyume na taaluma yake,pia kitamkumbusha kuzingatia thamani ya fedha,usalama wa maisha ya binadamu na mazingira,kutoruhusu masuala ya jinai,kidini,jinsia,ukabila,rangi,milengoya kisiasa katika kutekeleza kazi zake za uhandisi”amesisitiza Prof. Mwinyiwiwa

Amesema katika majadiliano kitaaluma mada kuu itakuwa ni athari za mapinduzi ya nne ya viwanda kwenye miundombinu kwa uendelevu wa uchumi wa kati.

“Pia zitakuwepo mada ndogo kamavile mafunzo na kujenga uwezo,miundombinu na maendeleo ya viwanda, namna na mbinu za kuhimili msongo wa mawazao kwa afya njema”amesema Prof. Mwinyiwiwa.

Amesema  katika maadhimisho hayo kutakuwa na  utoaji wa tuzo kwa wahandisi na wahitimu wa taasisi.

“Hii ni moja ya shughuli kubwa itakayofanyika wakati wa kuadhimisha siku ya wahandisi kwa mwaka huu bodi itatoa tuzo kwa makundi ya wahandisi wahitimu kutoka vyuo vikuu na taasisi za uhandisi nchini mwaka 2019/20″amesema.

Amesema   tuzo hiyo itakuwa ni kwa ajili ya taasisi iliyofanya vizuri katika  maonyesho ya teknolojia na ubunifu, katika maonyesho ya biashara,taasisi iliyotia fora kwenye maonyesho ya huduma za kitaaluma na taasisi iliyotia fora kwenye maonyesho ya uchuuzi.

Vilevile, amesema  maadhimisho hayo yanatarajiwa kuhuduriwa na watu zaidi ya 3,500 na wengine 2,000 watashiriki kwa njia ya mtandao kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Msajili bodi ya usajili Wahandisi nchini Patrick Barozi, amesema hadi sasa wahandisi 17, wamechukuliwa hatua za kinidhamu kwa makosa mbalimbali.

Amesema  moja katika makosa ambayo yameonekana kufanywa na wahandisi nchini ni kushindwa kusimamia kazi zao kwa viwango vilivyoelekezwa kwenye mikataba yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles