23.3 C
Dar es Salaam
Sunday, October 6, 2024

Contact us: [email protected]

KAMATI YA BUNGE YASHINDWA KUMUHOJI KUBENEA

Na RAMADHAN HASSAN -DODOMA

KAMATI ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imeshindwa kumuhoji Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema), baada ya mbunge huyo kubainika ni mgonjwa.

Kutokana na hali  hilo, Mwenyekiti wa kamati hiyo   George Mkuchika, alisema Kubenea alifikishwa mbele ya kamati akiwa kwenye akiwa kwenye kiti maalumu cha wagonjwa akilindwa na polisi.

“Kamati inakutana pale tunapoletewa mashauri na Mheshimiwa Spika kuhusu  suala la Mhe. Kubenea kudharau mamlaka ya Spika kwa kauli ambazo alitoa katika kanisa huko Dar es Salaam.

“Taratibu zetu zinataka kwamba ukiitwa mbele ya kamati unapelekewa na hati ya kuitwa ambayo Kubenea alishapelekewa. Alifika siku moja na kukubaliana tutafanya kikao saa tisa lakini alishindwa kwa sababu alilazwa hapa katika kituo cha afya bungeni.

“Polisi wamemleta hapa bungeni lakini akiwa katika baiskeli ya kusukuma wagonjwa na alipofika hapa alikuwa analalamika kuwa anaumwa.

“Ameiomba kamati impe muda akaendelee kupata matibabu  na kwamba afya yake ikishaimarika tumpangie siku nyingine.   Kutokana na hali iliyoonekana kamati imekubali maombi ya Mheshimiwa Kubeneka na kuagiza apelekwe mara moja  kwenye zahanati ya bunge na baada ya hapo yeye ataelekeza atakapatiwe wapi matibabu,” alisema Mkuchika.

Kubenea   aliwasili jana asubuhi mjini Dodoma huku akiwa chini ya ulinzi wa polisi.

Inadaiwa akiwa katika Kanisa la Askofu Josephat Gwajima, Dar es Salaam, alisema uongo kuhusu idadi ya risasi alizopigwa Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) Tundu Lissu katika tukio lililotokea nyumbani kwake Area D mjini Dodoma Septemba 7.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles