30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Kamati ya Bunge yafanya ukaguzi jengo la TIRDO

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo wamekagua na kuridhishwa na Maendeleo ya ujenzi wa jengo la Utawala la Taasisi ya Utafiti wa Viwanda na Maendeleo (TIRDO) lililogharimu Sh bilioni 3.4 ambapo linatajiwa kumalizika June 30, 2024.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 18, 2024 baada ya kukagua ujenzi huo, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Deodatus Mwanyika amesema Serikali imeongeza uwezo wa kimiundombinu TIRDO yenye majengo chakavu ambayo hayakuwa yanaendana na taasisi hiyo.

Amesema Serikali kupitia wizara hiyo iliidhinisha jengo la utawala litengenezwe kwani halijakamilika kwa muda mrefu.

“Jengo hili limeanza muda mrefu sana tangu 1984 na hapo katikati lilisimama sasa mnatakiwa likaimilike ili lianze kutumika kibiashara. Wizara muone haja ya kuwatumia watafiti wenu waliopo TIRDO kibiashara kama chanzo cha mapato,” Mwanyika.

Amesema wizara inapaswa kusimamia taasisi zake na kuhakikisha bajeti inayopangwa inatolewa kwa wakati ili kukamilisha mipango iliyowekwa.

Aidha ameshauri wizara kuweka kitengo ndani ya shirikisho kwa ajili ya ushauri wa kibiashara ili waweze kujitegemea.

Pia kamati hiyo imeitaka wizara ya viwanda na biashara kutoa fedha kukamilisha jengo la utawala wa TIRDO ili watafiti waweze kufanya kazi zao katika mazingira mazuri na ya biashara

Amesema taasisi hiyo ni muhimu kwa Serikali hasa kwenye sekta ya utafiti wa viwanda na uwanja wa sayansi na teknolojia.

Kwa upande wake Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Ashatu Kijaji amesema kwa hatua zilizobaki kukamilisha ujenzi wa jengo hilo, walikuwa na bajeti ya shilingi bilioni 3.4 ambapo hadi sasa wameshapokea shilingi bilioni 1.54 kwa ajili ya ukamilishani wa jengo hilo.

“Ili jengo likamilike bado tuna nusu fedha tunaendelea kuomba Serikalini kwa bajeti ijayo ili kukamilisha ujenzi huu hadi sasa umefikia asilimia 72 za mradi umebaki asilimia 28 na ujenzi huu unatarajia kukamilika June 30 mwaka huu,”amesema Dk. Kijaji.

Aidha ameishukuru kamati hiyo kwa kuweza kuisukuma Serikali na hatimae kupatikana kwa fedha hizo na ujenzi ukiendelea kutoka asilimia 50 iliyokuwepo mwaka jana na kufikia asilimia 72.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles