26.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu yampongeza Mkurugenzi Mkuu TPA

 Na Mwandishi Wetu, Mwanza

Kamati ya   Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imempongeza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA), Plasduce Mbossa kwa kusimamia vyema miradi mbalimbali ya kimkakati ya sekta hiyo inayotekelezwa na serikali katika maeneo mbalimbali nchini.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakikagua mradi wa upanuzi na ufanyaji wa maboresho ya bandari ya Mwanza Kaskazini.

Pongezi hizo zimetolewa na kamati hiyo jijini hapa Machi 16,2024 baada ya kutembelea na kukagua mradi wa upanuzi na ufanyaji  wa maboresho ya bandari ya Mwanza Kaskazini unaojengwa na serikali kwa gharama ya Sh bilioni 18.6  ambao ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 30.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Seleman Kakoso amesema Serikali imewekeza fedha nyingi ambazo zinajenga na kuboresha bandari mbalimbali nchini zinazosimamiwa  na TPA, miradi yote iko katika hatua nzuri za utekelezaji kutokana na usimamizi mzuri chini ya uongozi wa  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Plasduce Mbossa. 

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Plasduce Mbossa.

“Mradi huu ni mradi wa kimkakati ambao serikali imewekeza fedha nyingi, Mheshimiwa  Rais Samia Suluhu Hassan ametoa fedha kwa ajili ya upanuzi wa bandari ya Dar es Salaam, ametoa fedha nyingi kwa ajili ya kujenga bandari kavu ya kwala na miradi yote kwa kweli inasimimiwa vizuri sana na TPA.

“Ingawa Mkurugenzi wa TPA ni kijana mdogo lakini hakika utendaji na uwajibikaji wake tunauona anachapa kazi kwelikweli ni mzalendo rai yangu kwa vijana wengine wakipewa nafasi waige mfano wa Mbossa,”amesema Kakoso.

Kwa upande wake Meneja wa Bandari za Kanda ya Ziwa, Erasto Lugenge amesema utekelezaji wa mradi huo unaendelea vizuri, wanatarajia utakamilika kwa muda uliopangwa kwa kuwa serikali inaendelea kutatua changamoto mbalimbali zinazoukabili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles