28.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

Kada ya Uuguzi na Ukunga yaiomba Serikali kuharakisha mapitio ya mapendekezo yake

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Kada ya Uuguzi na Ukunga nchini imeiomba Serikali kupitia Wizara ya Afya kuharakisha mapitio ya mapendekezo yake juu ya maboresho pendekezwa ya mgawanyo wa madaraka sawa kwenye ngazi zote kwa kuzingatia vigezo vya elimu na weledi.

Hayo yamejiri Jijini hapa kwenye Jukwaa la mwaka linalowakutanisha wauguzi na wakunga Machi 18, 2024 kwa lengo la kufanya tathimini ya utekelezaji wa utendaji kazi wa utoaji wa huduma za uuguzi na Ukunga ambapo zoezi hilo lililoenda sambamba na uzinduzi wa jarida la idara ya Uuguzi na Ukunga jijini Dodoma.

Akiwasilisha mapendekezo hayo kwa Naibu Waziri wa Afya, Dk. Godwin Mollel,Katibu wa Kada hiyo Moses Tawete amesema ikiwa mapendokezo hayo yatafanyiwa kazi itasaidia kuondoa mtizamo uliopo sasa wa taaluma moja kuhodhi nafasi zote katika sekta ya Afya.

Tawete ameshauri pia zoezi la uongezaji wa vituo vya Afya uendane na ajira mpya ili kukidhi utoaji huduma kwa jamii ikiwa ni pamoja na kuwekeza zaidi kwenye vifaa tiba.

Suala la maboresho ya mfuko wa Taifa wa bima ya Afya(NHIF)halikuachwa nyuma ambapo amependekeza kuwa kitika cha mafao kijumuishe huduma za Ukunga na Uuguzi kwa manufaa ya wananchi wa hali ya chini.

Kutokana na hayo,Naibu Waziri wa Afya Dk. Godwin Mollel amesema Serikali itaangalia namna bora ya kuboresha mapendekezo hayo huku akieleza kuwa Kada hiyo ni muhimu kwa jamii na hivyo inatakiwa kuwezeshwa ili ifanye kazi kwenye mazingira mazuri.

Amesema asilimia 60 ya watumishi katika sekta ya afya nchini wanatoka kada za uuguzi na ukunga hivyo kuchangia ubora wa huduma zinazotolewa katika Hospitali na Vituo vya kutolea huduma za afya.

Dk. Mollel amesema kada ya Uuguzi imekuwa muhimu katika kutoa huduma bora kwa sababu asilimia 80 ya kazi za afya zinatekelezwa na kada hiyo na kutoa rai kada hiyo kujumuishwa kwenye mfumo wa utoaji wa maamuzi.

Ameongeza kuwa,”Ukiona kituo cha afya kinatoa huduna bora ni kwa sababu ya uwepo wa wauguzi ambao ndio wamekuwa watendaji wakuu ambao wanakaa muda mwingi na wagonjwa hivyo ni muhimu wakawekwa kwenye mfumo wa uongozi na utoaji wa maamuzi na uundwaji wa sera,” amesema Dk. Mollel

Ameongeza kuwa wauguzi na wakunga wanapopata fursa ya kuingia ndani ya mfumo wa uongozi watasaidia kuhakikisha mambo yanaboreshwa kwenye sekta ya Afya lakini pia maslahi yao Kwa upande wake Mkurugenzi wa idara ya Huduma za Uuguzi na Ukunga,

Ziada Sella ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kuajiri Wauguzi na Wakunga zaidi ya 40,000 kwa kipindi cha mwaka 2022/2023 na kuongeza kuwa kada hiyo ina dhamana kubwa katika utoaji wa huduma hivyo wazingatie miongozo, kanuni na sheria zilizowekwa kwa maslahi ya taifa.

“Tunamshukuru Rais wetu Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kibali cha kuajiri wauguzi na wakunga zaidi ya elfu arobaini hii inaonyesha umuhimu na dhamana ya kada hii kwa sababu hawa ndio hutumia muda mwingi kukaa na wagonjwa.

Kwa upande wake Rais wa Chama cha Manesi, Alexander Balunya amesema pamoja na kubeba jukumu zito kwenye jamii Kada hiyo bado haipewi kipaumbele na kuiomba Serikali kuhakikisha inatatua kero zote na kuweka uwekezaji unaohitajika.

“Huduma za Uuguzi ni mtambuka hivyo wanahitaji usimamizi wezeshi, muundo wa utawala unapaswa kufanyiwa mapitio ili kuwa na muundo unaiwatambua hata pale wanapotoka kujiendeleza, hili likifanikiwa litaongeza chachu ya utoaji huduma za Ukunga na Uuguzi kwa jamii,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles