25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 7, 2024

Contact us: [email protected]

Wanahabari washauriwa kuvaa mavazi yanayowatambulisha kwenye maeneo hatarishi

Na Malima Lubasha, Musoma

JESHI la Polisi mkoani Mara limetoa ushauri kwa Waandishi wa Habari kuvaa mavazi ya kuwatambulisha wakati wanapokuwa wanatimiza wajibu wao maeneo hatarishi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, ACP Salimu Morcase ametoa ushauri huo kwenye mdahalo kuhusu ulinzi na usalama kwa waandishi wa habari wakati wa kuwasilisha ujumbe wake wa jeshi la polisi uliofa nyika Hoteli mjini musoma.

Katika ujumbe wake uliowasilishwa na msaidizi wa kamanda wa mkoa, Thomas Makene amesema waandishi wa habari wanapaswa kutimiza majukumu yao wakiwa salama ili wananchi waweze kupata taarifa mbalimbali kuhusu maendeleo yao na changamoto nyingine.

Amesema Jeshi la Polisi pia linapaswa kumlinda mwandishi wakati anatekeleza majukumu yake lakini akiwa kwenye maeneo hatarishi anapaswa kuwa na vazi maalum la kumtabulisha.

Makene amesema kuwa yapo maeneo ambayo mwandishi anaweza kuwa anatimiza wajibu wake na ikitokea vurugu ambazo anatakiwa kulindwa kwani anapokuwa na vazi maalum la kumtambulisha inaku wa ni salama zaidi kwa kumlinda na kumtoa kwenye hatari.

“Mdahalo huu unaongeza mahusiano mazuri baina ya jeshi la polisi na waandishi wa habari katika kufahamiana zaidi na kujenga ushirikiano,” amesema.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mara (MRPC), Raphael Okelo, amesema kuwa kwa sasa kumekuwa na mahusiano mazuri baina ya Mwandishi wa Habari na Jeshi la Polisi.

Okelo amesema huo ni mdahalowa 4 tangu kuanza kufanyika na imekuwa na mafanikio na kuimarisha mahusiano katika majukumu ya kazi kwa pande zote mbili ambapo mdahalo huo ulishirikisha waandishi wa habari, jeshi la polisi,asasi za kiraia,wanasheria na viongozi wa dini.

Hata hivyo kwa nyakati tofauti waki changia mdahalo huo kuhusu Ulinzi na Usalama kwa waandishi wa Habari,Jeshi la Polisi baadhi ya washiriki walisisitiza waandishi kuzingatia weledi taaluma na sheria kuhusu sekta hiyo kwa kuvaa vazi la kuwatambulisha maeneo hatarishi wakati wanatimiza wajibu wao itaka yosaidia kuepuka hatari na kuondoa migongano.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles