26.9 C
Dar es Salaam
Friday, December 9, 2022

Contact us: [email protected]

Joto la uteuzi lazidi lapanda

 FARAJA MASINDE NaANDREW MSECHU

JOTO la Uchaguzi mkuu limezidi kupanda, huku vyama vikubwa vya siasa vikijifungia kwa ajili ya kuteua wagombea wa nafasi mbalimbali, ikiwemo urais na ubunge.

Kuanzia jana, viongozi wa Chama cha Domokrasia na Maendeleo (Chadema) na viongozi wakuu wa Chama cha ACT Wazalendo walianza vikao vya ndani katika meneo tofauti kwa ajili ya Kamati Kuu, kisha Halmashauri Kuu na hatimaye mkutano mkuu ambavyo kwa pamoja vinatarajiwa kukamilika keshokutwa.

Vikao hivyo ndivyo vitapitisha majina ya wagombea wa nafasi hizo muhimu.

Kwa upande wa Chadema wamekuwa wakindeela na vikao katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam, wakati ACT Wazalendo wakiwa kwenye ukumbi wa Lamada ambapo miongoni mwa agenda kuu ni kupitisha majina ya wagombea urais na wagombea wa ubunge.

Wakati vyama hivyo vikiendelea kujipanga kwa ajili ya kupata wagombea watakaoviwakilisha kwenye uchaguzi wa rais, wabunge na madiwani Oktoba, mwaka huu, pia vimekuwa katika mchakato wa kuangalia namna vinavyoweza kushirikiana kwa kusimamisha mgombea mmoja wa urais.

Tayari Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimeanza vikao vya Kamati za Siasa za Wilaya tangu Agosti mosi na kesho ni zamu ya Kamati za Siasa za Mikoa kuendelea na vikao vya kupitia sifa za wagombea wote wa ubunge.

Baada ya vikao hivyo taarifa za wagombea wote zitapelekwa makao makuu Dodoma kwa ajili ya uamuzi wa mwisho wa uteuzi.

USHIRIKIANO

Vimekuwa katika mchakato wa kuangalia namna vinavyoweza kushirikiana kwa kuungana mkono katika nafasi za urais, ubunge na udiwani, kulingana na kukubalika kwao maeneo husika.

Ushirikiano huo,unatarajia kuchukua nafasi ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ambao uliviunganisha vyama vya Chadema, CUF, NCCR Mageuzi na NLD, ambavyo kwa pamoja vilikubalina kuungana mkono wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Akizungumzia nafasi ya vyama kushirikiana, Naibu Mwenyekiti Itikadi, Uenezi na Mawasiliano kwa Umma wa ACT Wasalendo, Janeth Rithe alisema jana chama chake kiko tayari kushirikiana na vyama vyenye malengo yanayofanana ili kuhakikisha wanashinda katika uchaguzi mkuu ujao.

Alisema wakati vikao vya ndani vya Kamati Kuu, Halmashauri Kuu na Mkutano Mkuu vya chama hicho vikiendelea kuanzia jana na kuhitimishwa Agosti 5, mwkaa huu, suala la kushirikiana na miongoni mwa mambo yatakayojadiliwa.

Alisemas ni wazi kwa sasa suala la kushirkiana miongoni mwa vyama vya upinzani dhidi ya CCM ni la muhimu, chama chake kinalichukua hilo kwa namna na umuhimu wa kipekee.

“Katika suala la ushirikiano baina ya vyama kwenye uchaguzi mkuu ujao, tunatambua na kuheshimu umuhimu wa ushirikiano baina ya vyama kwenye nafasi zote. Tunavyozungumza kuna mazungumzo yanayoshusisha viongozi na wataalamu wa vyama amabayo yanbaendelea.

“Sisi tunaona ushirikiano ni suala la muhimu sana,tunaona ni vizuri ukihusisha vyama vyote vyenye malengo kama yetu katika upinzani. “Wakati mazungumzo yanaendelea, kila chama kinaendelea kupitisha wagombea wake katika nafasi mbalimbali za urais, ubunge na udiwani.

“Makubaliano yakishafikiwa na timu zetu za mazungumzo tutakaa tuangalie ni maeneo yapi ya kuachiana. Tunaamini mazingira ya ushirikiano yataangalia zaidi maslahi ya nchi na si maslahi ya mtu mmoja mmoja au chama kimoja kimoja,” alisema.

Alisema ACT Wazalendo ina matumaini suala hilo litapatiwa suluhisho kuhusu ni namna gani watashirikiana na idadi ya vyama vitakavyoshirikiana kwa ajili yakusimamisha mgombea mmoja wa urais na kuangalia namna ya kugawana majimbo kulingana na maeneo ambayo vyama hivyo vina nguvu.

Alisema anaamini timu ya majadiliano inayoendelea na kazi yake itakuwa na majibu mazuri ya mapema wakati vyma,vinapokwenda kuhirimisha taratibu zake mikutano na uteuzi inayoendelea na inayotarajiwa kumalizika wiki hii.

MSIMAMO WA CHADEMA

Wakati ACT Wazalendo ikieleza utayari wake, Chadema ambacho jana kilianza vikao vyake vya Kamati Kuu kwa ajili ya kuchuja wagombea na kufuatiwa na vikao vya Halmashauri Kuu na Mkutano Mkuu kilieleza utayari wake katika suala la ushirikiano na vyama vingine.

Katika mkutano wake wa Juni 3, mwaka huu, Katibu Mkuu John Mnyika alisema chama chake kimefugua milango ya majadiliano na vyama vingine vya siasa,hasa vile vyenye dhamira ya kweli kushirikiana kuiondoa CCM madarakani. 

Alisema haoni dalili kama ushirikiano wa mwaka 2015 chini ya Ukawa utaendelea, na bado hawajajua ni vyama gani na vingapi vitakuwa tayari kushirikiana.

Ugumu wa Ukawa kuendeela kuwepo mwaka huu unatokana na mwelekeo wa vyama viwili ambavyo vilishiriki kuunda umoja huo, yaani NCCR Mageuzi na CUF ambavyo vinaonekana kujiweka kando.

Katika siku za hivi karibuni, NCCR-Mageuzi, imekuwa ikiwachukua wabunge kutoka Chadema, huku mwenyekiti wake, James Mbatia kikaririwa wa mara kadhaa akieleza umoja wa Ukawa haukuwa na manufaa kwa chama chake. Wabunge wa Chadema waliohamia NCCR Mageuzi,ni Anthony Komu (Moshi Vijijini), Joseph Selasini (Rombo), na wabunge wawili wa viti maalumu, Susan Maselle na Joyce Sokombi.

Kwa upande wa chama cha CUF ambacho mwaka 2015 kilishiriki Ukawa, kiliingia katika mgogoro wa ndani na kusababisha aliyekuwa katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad na wale waliokuwa wakimuunga mkono kuhamia ACT Wazalendo.

Mgogoro huo, ulisababishwa na aliyekuwa Mwenyekiti wake, Profesa Ibrahim Lipumba ambaye alijiuzulu uenyekiti muda mfupi kabla ya uchaguzi kisha kurejea baada ya uchaguzi na kuibua mgogoro ndani ya chama hicho, suala linalofanya ushirikiano wa chama chake na Chadema kwa sasa kutopewa nafasi kubwa.

Ushirikano wa sasa wa vyama unaungwa mkono na vyama cvya Chadema, ACT Wazalendo, Chauma, na vyama vingine visivyo na wabunge ambavyo vimeonesha nia ya kuingia katika ushirikiano huo.

Hivi karibuni kumekuwa na ushirikiano wa vyama 15 vya siasa nchini kupitia viongozi wake wakuu, ambavyo mara kadhaa vimekuwa vikikutana na kutoa matamko ya pamoja kati8ka mambo kadhaa, ikiwemo kuhusisa na kupinga muswada wa mabadiliko ya sheria ya vyama vya siasa uliowasilishwa bungeni na kupitishwa wakati wa mkutano wa 13 wa bunge la 11 jijini Dodoma.

Vyama ambavyo vimekuwa vikishiriki katikaushirikiano huo ni ACT Wazalendo, CUF, UPDP, DP, CCK, Chadema, Chauma, NCCR Mageuzi, NLD na ADC.

Katika hatua nyingine Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan amefichua siri ya tumbuatumbua inayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dk. John Magufuli kuwa ni kutokana na wateule hao kukosa maadili na heshima kwenye nafasi wanazoteuliwa.

Makamu wa Rais aliyasema hayo jana wakati akifunga kongamano la Wanawake linalofahamika kama Girl Power liliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julias Nyerere (JNICC) Dar es Salaam.

Alisema kukosekana kwa maadili na heshima za utendaji ndiyo imekuwa sababu ya viongozi mbalimbali kutenguliwa kwenye nyadhifa zao.

“Kukosekana kwa maadili na nidhamu ndiyo maana tunasikia watu wanatumbuliwa, ni kutokana na kukosa maadili na heshima kwenye majukumu yao.

 “Hivyo usipojishusha leo ndiyo maana hata mbele ya safari ukifanya kazi ukafika wakati ukasema unataka ukasake jimbo ugombee watu watafuatilia historia yako ya nyuma kisha wanakuacha kwa kuwa haufai,” alisema Samia.

Aliwataka wasichana na wanawake kuishi kwa kuzingatia maadili, heshima na kumtanguliza Mungu kila wakati, pia wakizingatia suala zima la elimu.

“Hata mimi nilikuwa na malengo, hivyo pamoja na kwamba sikufanya vyema kidato cha nne lakini hakunikatisha tamaa, nilipambana kwa kumuani Mungu na leo niko hapa japo ni lazima nikiri kwamba sikuwahi kuwa na ndoto ya kuja kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania wala sikutegemea, ni uweza wa Mumngu tu.

“Nakumbuka wakati tuko kwenye Bunge la Katiba, Paul Makonda alisema kabisa kwamba jamani wagombea urais ikiwapendeza huyu mama akawe Makamu wa Rais, na katika hilo namshukuru Mungu kwamba mkuu wangu ananiamini na amekuwa hana mashaka na mimi hata kidogo linapokuja utendaji kazi na ndiyo maana akanipa nafasi tena, hii ni maadili na nidhamu tu,” alisema Samia.

Alisema wanawake ni raslimali ambayo bado haijatumika duniani jambo ambalo aliwataka kuamka na kuchangamkia fursa kwa kuwa ni watu wenye nguvu kubwa ikiwamo kikatiba na kisheria.

 “Kazi yetu ni kujitokeza kwa wingi ili tuweze kutumika kikamlifu katika maeneo tofautitofauti, tuinuke tunaona fursa zilizopo ili twende mbele bila kusubiri kutegemea kuitwa” alisema Samia.

Awali, Rais Dk. Magufuli alipiga simu kwenye tamasha hilo na kusema kuwa anatamani kuona likiendelea kufanyika kila mwaka.

“Nimefurahi sana akina mama wale na dada zetu, nimefurahi sana kwa kweli mnaweza, nimekuwa nikiwafutilia mara zote mlipokuwa hapa kwa kweli mnaweza na ssiku nyingine mnikaribishe namimi nije hapo.

“Kwa kweli sitawaacha wala sitawaangusha, mmenifurahisha sana najisikia raha, Mungu awajalie sana. Nimeona wanawake wenye uwezo mkubwa, tuko pamoja na nimefurahia kipindi hiki ni kizuri kinatakiwa kiendelezwe ili tujue vipaji vya wanawake kwenye taifa hili,” alisema Rais Magufuli.

Katika tamasha hilo wanawake katika fani mbalimbali walijitokeza katika kuhakikisha kuwa wanawapa moyo wasichana na wanawake wengine kuthubutu na kutimiza ndoto zao.

Miongoni mwao ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dk. Zainabu Chaula ambaye amefanya kazi katika sekta mbalimbali ikiwamo wizara ya afya.

 “Siri ya mafanikio yangu pamoja na kumshukuru Mungu, ni jamii inayonizunguka, tupo watoto 20, Baba yangu anamiaka 90 na Mama yangu alifariki mwaka 2018.

“Hivyo safari yangu yote nimetembea na wanafunzi wenzangu kwani tulikuwa tunashirikiana, pia nilienda jeshini mwaka 1987, baadaye nikajiunga na Chuo Kikuu cha Dar ea Salaam na nikabahatika kuolewa nikiwa mwaka wa kwanza na mume wangu ni Daktari, hivyo changamoto kubwa ni namna ya kuishi na kushirikiana na watu,” alisema Dk. Zainabu.

Alisema siri ni kuipenda kazi yake na kuwapenda wagojwa, jambo la msingi ni kuwapa moyo wengina na kuwafundisha kile unachokijua.

“Niliamini katika uchambuzi wa mambo kwa kuwa napenda, hivyo baada ya kuteuliwa nilijifunza kwa wale niliowakuta pale Tamisemi, alitumia miezi miwili baada ya iteuzi, baadaye akabainisha ukweli alioubaini,” alisema.

Mwingine ni Profesa Neema Mollel ambaye ni Profesa mdogo zaidi nchini ambaye alisema siri ya yeye kuwa na wadhfa huo ni kuamini kwamba ina wezekana kwa kila anayeamini.

“Kutokana na maisha ambayo nimewahi kuyapitia nilikuwa naamini sana kwamba mimi naweza kuwa mwalimu na naweza kuwa Profesa, pia kutokana na malezi niliyolelewa ya wazazi wangu kuwa walimu hata mimi nilitamani japo matamanio yangu yalikiwa kuwa zaidi ya wao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,735FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles