28.7 C
Dar es Salaam
Monday, October 25, 2021

JANUARY ATOA MAAGIZO HOTELI ZA KITALII

Na DENNIS LUAMBANO- NGORONGORO


WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba, ametoa agizo kwa hoteli tisa za kitalii, loji na kambi za kudumu za watalii zilizopo ndani na nje ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), kuacha kutumia maji ya mito na mabwawa yanayopatikana ndani ya kreta ya Ngorongoro.

Akizungumza mjini hapa juzi katika mkutano na wajumbe wa Baraza la Wafugaji wa Hifadhi ya Ngorongoro ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kukagua shughuli za uhifadhi wa mazingira na athari za mabadiliko ya tabianchi, January alisema anatoa kipindi cha mpito cha miezi sita na baada ya hapo wenye hoteli hizo watafute vyanzo vingine vya maji vilivyopo nje ya kreta hiyo kwa matumizi yao na wateja wao.

“Natoa miezi sita tu kuanzia sasa na baada ya hapo wawekezaji wa hoteli hizo waanze kutumia maji kutoka vyanzo vingine vilivyopo nje ya kreta.

“Wenye hizo hoteli wana fedha, kwa hiyo hawawezi kushindwa kuvuta maji kutoka katika vyanzo vingine vilivyopo nje ya kreta, waende hata katika chanzo cha opusare.

“Tumeamua kuchukua hatua hizi kwa nia nzuri kabisa ya kutunza mazingira kwa sababu kuna msitu mmoja upo ndani ya kreta umepotea kwa sababu unakosa maji kwani yanavutwa na kupelekwa katika hoteli hizo,” alisema.

Pamoja na agizo hilo, alitoa agizo jingine la miezi sita kwa NCAA akitaka iandae ramani ya kreta inayoonyesha vyanzo na inapoelekea vijito, mito na mabwawa yaliyopo ndani ya kreta hiyo.

Pia aliliagiza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), kuzipiga faini hoteli sita kati ya hizo ambazo hazina vyeti vya tathmini ya athari za mazingira.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
163,099FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles