22.7 C
Dar es Salaam
Sunday, June 4, 2023

Contact us: [email protected]

JAMHURI KUMLETA MPENZI NONDO KUTOA USHAHIDI

Na Raymond Minja Iringa

Upande wa Jamhuri katika kesi ya Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo, Veronica Fredy anatarajiwa kuletwa makamani kutoa ushahidi katika kesi inayomkabili mwanafunzi huyo.

Mbali na mpenzi huyo wa Nondo, Jamhuri pia inakusudia kuleta mashahidi wengine wanne ambao ni Koplo Salum, Alphonce Mwamule, Koplo Abdulkadir na mfanyakazi kutoka Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo.

Kesi hiyo ilikuja leo mbele ya hakimu Mkazi wa Wilaya ya Iringa, John Mpitanjia kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali ambapo Wakili wa Serikali, Abel Mwandalamo amesema Nondo anakabiliwa na mashtaka mawili ambayo ni kusambaza taarifa za uongo akiwa Ubungo jijini Dar Es Salaam na kutoa taarifa za uongo akiwa mjini Mafinga kwa askari Polisi kituo cha Mafinga Wilayani Mufindi.

Wakili Mwandalamo amedai upande wa Jamhuri unakusudia kuambatanisha vielelezo vya ushahidi ambavyo ni taarifa za uchunguzi kuhusiana na mawasiliano ya simu, maelezo kutoka Mjini Mafinga yakidai Nondo katekwa na kuleta kielelezo cha simu za mkononi.

Hakimu Mpita Njia ameahirisha kesi hiyo hadi Aprili 18, mwaka huu ambapo itaanza kusikilizwa kwa siku mbili mfululizo, kutokana na maombi ya upande wa utetezi ya Wakili Charles Luoga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,283FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles