27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

‘POWER BANK’ YA MBUNGE CHANZO CHA MOTO BUNGENI

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

Bunge limetoa ufafanuzi kuhusu moshi uliotanda na kuzua taharuki jana bungeni na kusababisha bunge kuahirishwa kabla ya muda wake

Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson amesema chanzo ni ‘power bank’ iliyokuwa ikichaji simu mbili kwa wakati mmoja kwenye droo ya meza ya Mbunge Nsimbo, Richard Mbogo.

Dk. Tulia amesema tukio hilo lilitokea saa 1:20 usiku wakati kikao cha bunge kikiendelea ambapo ulitokea mlipuko wa kifaa cha kielektroniki cha kuchajia simu ya mkononi (power bank) na kusababisha harufu kali iliyotanda kutanda moshi katika ukumbi wa bunge hasa upande wa kulia wa kiti cha Spika.

“Kwa mujibu wa maelezo ya askari wa Bunge mlipuko ulitokea kwenye power bank ambayo ilikuwa ikichaji simu mbili kwa wakati mmoja kwenye droo ya meza ya Mheshimiwa Mbogo
ambapo kifaa hicho kiliteketea kwa moto, kuanguka chini na kuunguza zuria na pembeni mwa kiti cha mbunge huyo.

“Katika tukio hilo hakukuwa na majeruhi isipokuwa baadhi ya wabunge walipata mshtuko na baadhi yao walikimbia nje ya ukumbi wa bunge na waliobaki ndani ya ukumbi walipaliwa na moshi na kuanza kukohoa,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles