27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

CHANJO SARATANI YA KIZAZI YAZINDULIWA RASMI

Na Veronica Romwald, Dar es Salaam

Hatimaye Tanzania leo imeandika historia katika sekta afya baada ya kuzindua rasmi chanjo ya kuwakinga wasichana dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi (HPV).

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan amezindua chanjo hiyo leo katika viwanja vya Mbagala zakheim, Temeke, jijini Dar es Salaam ambapo amesema tatizo la saratani nchini limekuwa likiongezeka na kukua kila mwaka.

“Takribani wagonjwa wapya 50,000 hugundulika na saratani za aina mbalimbali, kwa bahati mbaya ni wagonjwa 13,000 tu kati ya hao, sawa na asilimia 26 ambao hufanikiwa kufika hospitalini kwa matibabu,” amesema.

Amesema saratani ya mlango wa kizazi ndiyo inayoongoza kuwa na wagonjwa wengi kwa asilimia 32.8 na huchangia asilimia 38 ya vifo vyote vitokanavyo na saratani nchini.

“Hata hivyo, wataalamu wanatueleza kwamba saratani hii inazuilika, hii ni habari njema kwetu na mojawapo ya njia zilizothibitishwa kuwa na uwezo mkubwa wa kuzuia saratani ni utoaji wa chanjo hii ya HPV.

“Kwa mwaka huu, tunakusudia kutoa chanjo kwa jumla ya wasichana 616,734 wa umri wa miaka 14,” amesema.

Awali, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema chanjo hiyo itatolewa bila malipo.

“Niwahakikishie Watanzania kwamba chanjo hii imethibitishwa kwamba ni salama kwa matumizi ya binadamu,” amesisitiza

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles