24.8 C
Dar es Salaam
Friday, June 2, 2023

Contact us: [email protected]

JACQUELINE JOSSA AACHWA AKIWA MJAMZITO

LONDON, ENGLAND


NYOTA wa filamu nchini England, Jacqueline Jossa, amethibitisha kuachana na baba wa mtoto wake, Dan Osborne, ikiwa ni mwaka mmoja tangu wafunge ndoa.

Wawili hao walifunga ndoa mwaka jana na tayari walifanikiwa kuwa na mtoto wa kwanza wa kike ambaye anajulikana kwa jina la Ella. Wamekuwa kwenye uhusiano kwa kipindi cha miaka minne.

Kupitia ukurasa wa Twitter, Jacqueline, aliandika ujumbe wa kuthibitisha kuachana kwao. “Hakuna sababu ya watu kuingilia vitu ambavyo hawavijui, lakini naomba niweke wazi kuwa mimi na Daniel tumekuwa tukifanya mambo yetu kwa siri sana na kila stori lazima iwe na sehemu mbili, hivyo nitashangaa kuona watu wanazungumza vitu ambavyo hawavijui.

“Kinachobaki kwa sasa ni kwamba, sisi ni wazazi, hivyo tutabaki kama wazazi kwa ajili ya watoto wetu na tunaendelea kusapotiana kwa kila namna kama tulivyokubaliana,” alisema Jacqueline.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,264FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles