22.8 C
Dar es Salaam
Saturday, June 3, 2023

Contact us: [email protected]

KYLIE: STORMI AMEBADILISHA MAISHA YANGU

NEW YORK, MAREKANI


MAPEMA Februari mwaka huu, mwanamitindo maarufu nchini Marekani, Kylie Jenner, alifanikiwa kupata mtoto wake wa kwanza na kumpa jina la Stormi, hivyo mrembo huyo ameweka wazi kuwa maisha yake yamebadilika kwa kiasi kikubwa kutokana na mtoto huyo.

Mrembo huyo amedai amekuwa akitumia muda mwingi kuangalia maendeleo ya mtoto wake na kuacha kufanya mambo mengine kama ilivyo awali.

“Nimejifunza mambo mengi tangu nilipofanikiwa kuwa na mtoto, kuna wakati mambo yanafurahisha na mengine yanashangaza, lakini hadi sasa naweza kusema nimekuwa na uzoefu mkubwa na maisha yangu kwa ujumla yamebadilika.

“Mwanzo nilikuwa katika wakati mgumu kwa kuwa kuna wakati nilikuwa nakosa kabisa usingizi kwa ajili ya mwanangu, hauwezi kulala wakati mtoto hana usingizi, hivyo nilikuwa namsubiri alale na mimi niweze kulala, lakini kuna wakati anaweza kulala muda mfupi akaamka na kuanza kulia, lazima uhakikishe unaenda sawa na kila kitu anachokitaka. Kutokana na hali hiyo, naweza kusema Stormi amebadilisha mfumo wa maisha yangu,” alisema Kylie.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,270FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles