31.2 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

SELENA AWAACHA NJIAPANDA MASHABIKI

LOS ANGELES, MAREKANI


HATIMAYE staa wa muziki nchini Marekani, Selena Gomez, ametangaza kuwa anatarajia kuachia wimbo wake mpya utakaojulikana kwa jina la ‘Back To You’, hivyo mashabiki wameshtushwa na jina la wimbo huo huku wakiamini labda anataka kurudiana na Justin Beiber.

Mrembo huyo alitumia ukurasa wake wa Instagram na kudai kuwa anatarajia kuachia wimbo huo Mei 10, mwaka huu.

“Wimbo wa ‘Back To You’ utakuwa tayari Mei 10, najua watu watajiuliza kwanini si video, lakini nimeamua kufanya hivyo kwanza ili watu wausikilize,” aliandika Selena.

Mashabiki wake wanaamini wimbo huo utakuwa unamhusu Bieber ambaye walirudiana mwaka 2017, lakini walikuja kuachana mapema mwaka huu na tayari Bieber ameonekana kutoka na mrembo mwingine akijulikana kwa jina la Baskin Champion.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles