Idadi ya waliokufa kwa tsunami yafikia 1,400

0
904

JAKARTA, INDONESIA

IDADI ya watu waliokufa kutokana na matetemeko ya ardhi na kimbunga cha tsunami nchini Indonesia imefikia 1,424.

Kwa mujibu wa shirika la kitaifa la kuratibu majanga, karibu watu 2,550 wamejeruhiwa vibaya.

Msemaji wa shirika hilo, Sutupo Nugroho ametoa takwimu hizo jana wakati akizungumza na waandishi habari mjini Jakarta.

Nugroho amesema bado kuna watu wengine waliofukiwa katika udongo na vifusi vya majengo yaliyoporomoka.

Wakati huo huo, shirika la kimataifa la msaada kwa watoto, Save the Children limesema kiasi ya watoto 600,000 wametenganishwa na wazazi wao kutokana na majanga hayo na wamepatwa na mshtuko.

Shirika hilo limesema watoto wengi wanalala mitaani na wengine kuachwa yatima na kwamba mashirika ya misaada yanashirikiana kwa karibu na serikali ili kuwatambua na kuwaunganisha watoto hao na ndugu zao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here