Jafo awaonya ma-RC, ma-DC, watumishi watakaochezea fedha sekta ya afya

0
1128

Bethsheba WamburaWaziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Seleman Jaffo, amewataka wakuu wa mikoa na wilaya kusimamia fedha zilizotolewa na Rais John Magufuli, kwa ajili ya sekta ya afya ili kazi zifanyike kwa ufanisi wakishirikiana wadau wa afya na wananchi.

Jafo ameyasema hayo leo Oktoba 5, alipokuwa akizungumza na viongozi wa wahudumu wa afya nchi nzima jijini Dodoma ambapo amesema anataka fedha hizo zielekezwe katika huduma za afya ili wahudumu wafanye kazi zao katika mazingira mazuri.

“Mtu yoyote atakayecheza na fedha hizo hata senti tano basi ajue hali yake itakuwa mbaya hatuwezi kuwa tunatoa fedha halafu hazifanyi kazi iliyokusudiwa,” amesema.

Aidha amewaagiza Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya Nchini kuhakikisha wanasimamia ukusanyaji wa mapato kwenye vituo vya afya  ili kuongeza mapato na kujiendesha vyenyewe.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here