23.2 C
Dar es Salaam
Friday, June 2, 2023

Contact us: [email protected]

HOSPITALI YA AGA KHAN DODOMA YATEKETEA KWA MOTO

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Hospitali ya Aga Khan (Apollo Medical Centre) iliyopo Barabara ya Sita mkoani Dodoma imeteketea kwa moto baada ya kutokea kwa hitilafu ya umeme.

Hitilafu hiyo ya umeme imesababishwa na kurejea ghafla kwa umeme saa tisa alasiri baada ya kukatika kuanzia saa mbili asubuhi leo Jumapili Februari 25.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ingawa amesema hajui chanzo cha moto huo.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto mkoani humo, amesema moto huo uliwaka kuanzia saa tisa na nusu ambapo hadi sasa unaendelea kuwaka huku jeshi la zimamoto likiendelea kuzima moto huo.

“Mimi nawalaumu wananchi kwani jengo limeungua saa tisa wao wametoa taarifa saa 11 jioni ambapo jeshi letu limefika hapa limekuta tayari moto umeunguza sehemu kubwa ya jingo,” amesema.

Hata hivyo, katika tukio hilo hakuna majeruhi huku wagonjwa waliokuwa wamelazwa hospitalini hapo wakihamishwa sehemu nyingine kuendelea na tiba.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,244FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles