26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

MATAIFA YA AFRIKA YANAONGOZA KWA UFISADI DUNIANI


BERLIN, UJERUMANI   |  

RIPOTI ya Shirika la Kimataifa la Kupambana na Ufisadi, Transparency International, limesema mataifa yaliyopo chini ya Jangwa la Sahara barani Afrika yanaongoza kwa ufisadi ulimwenguni.

Hali hiyo inaelezwa kutokea baada ya mataifa mengi kukokota juhudi zao zinapolikabili suala la ufisadi. Kwenye ripoti yake ya mwaka 2017, shirika hilo limesema limegundua maelezo yenye wasiwasi. Kaulimbiu ya Umoja wa Afrika ya mwaka huu ni; ‘Kushinda vita dhidi ya ufisadi, njia endelevu ya kubadilisha Afrika’.

Ripoti hiyo inaonesha mabadiliko na kutoa matumaini kwa mataifa ya Afrika. Mabadiliko katika mataifa ya Rwanda na Cape Verde yanaonesha kuwa ufisadi unaweza kudhibitiwa pakiwa na juhudi na nia njema. Matunda ya vita ya muda mrefu katika mataifa kama vile Cote d’ Ivore na Senegal yanaonekana.

Kwa upande mwingine vita dhidi ya ufisadi katika mataifa yaliyo chini ya orodha ya Shirika la Transparency International, kunaonyesha kuwa kibarua kigumu kwa mfano katika mataifa ya Sudan Kusini na Somalia.

Licha ya kuwa Afrika ina mataifa mengi ambayo yanakabiliwa na ufisadi, kuna baadhi ya mataifa yanayopiga hatua kama vile Botswana, Shelisheli, Cape Verde, Rwanda na Namibia yakilinganishwa na mataifa kama vile Italia, Ugiriki na Hungary. Botswana na Shelisheli yaliyo na alama 61 na 60 yamefanya vyema zaidi ya taifa kama vile Uhispania ambayo ina alama 57.

Katika Kanda ya Afrika Mashariki, Rwanda inaongoza huku ikiwa katika nafasi ya 48, Tanzania ni ya pili lakini ulimwenguni ni ya 103, Kenya ni ya tatu lakini ya 143 ulimwenguni. Uganda ni ya nne ikiwa ya 151 ulimwenguni na Burundi inashika nafasi ya 157 ulimwenguni. Sudan Kusini na Somalia ndio nchi zenye ufisadi zaidi ulimwenguni kati ya mataifa 179 na 180 ulimwenguni.

Shirika hilo lenye makao yake jijini Berlin, linasema licha ya kuwa pana juhudi za kukabiliana na donda hilo ulimwenguni, kasi ya mataifa mengi ni mdogo. Vile vile limesema kuwa; “kuikabili vita dhidi ya ufisadi huchukua muda mrefu, miaka sita baadaye mataifa mengi hayajapiga hatua.”

Ripoti hiyo imetolewa kutoka vyanzo 13, ikiwemo Benki ya Dunia, Benki ya Ustawi ya Afrika na Kongamano la Uchumi Ulimwenguni na kufanya uamuzi kutokana na viwango vya rushwa, ugavi wa fedha za umma, matumizi ya ofisi za umma kwa masilahi ya kibinafsi na masuala mengine ya ufisadi. Mataifa 180 yaliratibiwa kwenye utafiti huo.

Maeneo bora yalikuwa Ulaya Magharibi na wastani wa alama 66, huku eneo lililofanya vibaya zaidi likiwa ukanda wa mataifa ya Afrika yaliyo Kusini mwa Jangwa la Sahara likiwa na wastani wa alama 32, likifuatwa kwa karibu na Asia ya Kati iliyokuwa na wastani wa alama 34.

Kiwango cha wastani ulimwenguni ni alama 43. Kwa nchi za Ulaya, New Zealand na Denmark ziliongoza kwenye orodha hiyo zikiwa na alama 89 na 88, huku Somalia ikivuta mkia kwa alama tisa, kisha Sudan Kusini ikiwa na alama 12, Syria ikiwa na alama 14 na Afghanistan ikiwa na alama 15.

Uingereza ilitajwa kuwa moja ya mataifa yaliyoimarika kwa kipindi cha miaka sita na kuongeza alama zake kuwa nane tangu mwaka 2012 na kufikia alama 82 na kuiweka juu ya Ujerumani kwa alama moja na kukabana koo na Uholanzi, Luxembourg na Canada. Marekani imeshika nafasi sawa na Austria na Ubelgiji katika nafasi ya 16 kwa alama 75.

Shirika hilo limesema limekusanya takwimu kutoka kwa kamati ya kuwalinda wanahabari na kugundua kuwa wanahabari wamo hatarini kwenye mataifa fisadi.

Kwa miaka sita iliyopita, zaidi ya wanahabari 10 wameuawa katika mataifa yaliyo chini ya alama 45 na mmoja wa wanahabari kati ya watano alikuwa anafanya stori kuhusu ufisadi.

Mkurugenzi wa Shirika la Kimaitaifa la Transparency International, Patricia Moreira, amesema kampeni zenye kuchafua jina, dhuluma, ufisadi ni vyombo vinavyotumika na Serikali katika mbinu za kunyamazisha juhudi za kukabiliana na ufisadi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,225FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles