PROFESA SAFARI AONGEZA NGUVU KUMTETEA SUGU LEO

0
632

Na Upendo Fundisha, Mbeya

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Taifa, Profesa Abdalah Safari ameungana na Wakili Peter Kibatala na Faraji Mangula, kuwatetea washitakiwa hao leo wa kesi ya kutoa lugha ya fedheha dhidi ya Rais, inayomkabili  Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu), na Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga.

Kesi hiyo inaendelea hivi sasa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya huku ikihudhuriwa na viongozi wa juu wa chama hicho.

Mbali na Profesa Safari, viongozi wengine waliohudhuria kesi hiyo ambayo inatarajiwa kutolewa hukumu hivi punde ni Naibu Katibu Mkuu Taifa, John Mnyika na  Mwenyekiti Bavicha, Ole Sosopi.

Wengine ni wabunge Godbless Lema (Arusha Mjini), Mbunge wa Tunduma, Frank Mwakajoka, Mbunge wa Momba, David Silinde na Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here