23.9 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Henderson: Liverpool inahitaji miujiza

LONDON, ENGLAND

NAHODHA wa timu ya Liverpool, Jordan Henderson, amesema timu yake inaomba itokee miujiza kuipiku Machester City na kushinda taji la Ligi Kuu England msimu huu, huku ikitaka kutinga hatua ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.


Kabla ya Liverpool kuvaana na Wolves katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu England leo bila mshambuliaji wao, Mohamed Salah, itavaana na Barcelona katika mchezo wa hatua ya nusu fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Anfield, England.


Mchezo huo utachezwa baada ya mchezo wa kwanza Liverpool kufungwa mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Nou Camp Hispania.
Lakini Liverpool inaongoza Ligi Kuu England kwa tofauti ya pointi mbili dhidi ya Manchester City ambayo jana ilicheza dhidi ya Leicester City na kubakisha mchezo mmoja dhidi ya Brighton kumaliza ratiba ya ligi hiyo msimu huu.


Michezo yote itachezwa Mei 12, mwaka huu ambayo itaweka wazi bingwa wa ligi hiyo msimu huu.
Liverpool inatarajia Manchester City ipoteze pointi dhidi ya Leceister City inayofundishwa na kocha Brendan Rodgers ambayo ipo nafasi ya tisa katika msimamo wa ligi hiyo.


Henderson alisema timu yake inahitaji maombi maalumu kushinda mbio za ubingwa msimu huu.
“Liverpool ipo makini kufuatilia michezo ya Manchester City, ni kweli tunaiombea ipoteze,” alisema Henderson.


“Manchester City ni timu kubwa lakini hata sisi pia. Hata hivyo, kila mmoja wetu anastahili taji hilo hivyo tukilikosa wala hatutajilaumu.


“Tunakwenda kumaliza mchezo wetu wa mwisho na tunahitaji kumaliza katika kiwango cha juu huku tukiomba miujiza itokee tushinde taji hilo,” alisema Henderson.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles