21.4 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

Solskjaer kuwekwa kikaangoni Man Utd

MCHAMBUZI na mchezaji wa zamani wa Tottenham na Liverpool, Jamie Redknapp, anaamini Ole Gunnar Solskjaer muda wake kuendelea kukinoa kikosi cha Manchester United unahesabika.


Kauli hiyo inakuja baada ya Manchester United kukosa matumaini ya kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa msimu ujao, baada ya juzi kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Huddersfield.


Matokeo hayo yanaifanya Manchester United kushinda michezo miwili katika michezo 10 iliyopita tangu Solskjaer kuajiriwa moja kwa moja na klabu hiyo.


Redknapp anaamini Solskjaer kama atashindwa kufuzu michuano ya Europa Ligi pamoja na kusajili wachezaji wapya, anaweza kufukuzwa ndani ya klabu hiyo.


“Sipendi Solskjaer ashindwe kibarua chake lakini inaonekana kazi imekuwa kubwa kwake,” alisema Redknapp wakati akihojiwa na gazeti la Daily Mail.


“Hakuna anayefahamu kama Manchester United bado ipo kwenye mpango wake wa kumhitaji kocha Mauricio Pochettino wa Tottenham, lakini Mtendaji Mkuu, Ed Woodward, bado anaonekana kuwa na matumaini na kocha huyo.


“Solskjaer anaonekana kuwa na jina kubwa katika mchezo wa soka. Lakini ni miaka sita tangu Manchester United ishinde taji la Ligi Kuu England.


“Licha ya kazi kubwa aliyonayo mikononi mwake, atakuwa na presha wakati Manchester United ikitakiwa kushinda kila mchezo mbele yake baada ya timu hiyo kuwa nafasi ya sita kama ilivyokuwa Oktoba mwaka jana,” alisema.

Katika mchezo wa mwisho, Manchester United itacheza dhidi ya Cardiff City kwenye Uwanja wa Old Trafford Mei 12, mwaka huu. Katika mchezo huo, Solskjaer atawatumia wachezaji chipukizi wakati akijiandaa na nyota wa timu hiyo baada ya kushindwa kumshawishi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles