Hellen Sogia afafanua ‘You are Awesome God’

0
639

CHRISTOPHER MSEKENA

MWIMBAJI na mtumishi wa Mungu nchini, Hellen Sogia, amesema wimbo wake mpya, You Are Awesome God, ni miongoni mwa nyimbo zenye ujumbe mzuri unaomshukuru Mungu kwa kutupigania kila siku.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Sogia ambaye ni kiongozi wa huduma ya Oak Mission Ministry, alisema siku zote Mungu amekuwa akiwatetea, akiwapigania na kuwatendea makuu binadamu ndiyo maana alipata ufunuo wa kuimba wimbo huo wenye mguso wa kipekee.

“Mungu wetu ni mkuu sana, amekuwa akitupigania siku zote, binafsi nikayatazama matendo yake kwetu nikaona nisifu hadhi yake yeye aliyetuumba hadi leo hii tunaishi,” alisema Hellen.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here