DMX asitisha ziara, ajipeleka ‘rehab’

0
814

NEW YORK, MAREKANI

RAPA Earl Simmons maarufu kwa jina la DMX, ametumia ukurasa wake wa Instagram kuwatangazia mashabiki zake juu ya kusitisha kwake kwa ziara ya muziki na kuamua kwenda kupata matibabu ya afya yake ‘rehab’

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 48, amekuwa akisumbuliwa na afya yake kutokana na matumizi ya dawa za kulevya kwa kipindi kirefu.

“Kitu cha kwanza katika maisha yangu ni afya pamoja ya familia yangu, hivyo nimeamua kusitisha mipango yangu ya ziara ya muziki kwa ajili ya kuiweka sawa afya yangu, nitumie nafasi hii kuwaomba radhi mashabiki kwa usumbufu huo pamoja na kuwashukuru kwa sapoti,” aliandika msanii huyo.

Mwaka 2011, mtandao wa TMZ ulitoa taarifa kwamba, msanii huyo amekuwa akijiingiza kwenye dawa za kulevya kutokana na msongo wa mawazo juu ya kushindwa kuhudumia watoto wake, ana jumla ya watoto 10 hadi sasa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here