24.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 8, 2021

Hawa awakumbusha vijana dawa za kulevya

Beatrice Kaiza

MSANII wa muziki nchini, Hawa Mayoka ‘Hawa Nitarejea’ amesema kuwa kitu ambacho kinamumiza kwa sasa ni kuona vijana wanaingia kwenye dimbwi la utumiaji wa dawa za kulevya.

Akizungumza na MTANZANIA jana, alisema kuwa vijana wanatakiwa kujifunza kwa wale ambao wamepitia na kuteseka.

“Kitu ambacho siwezi kufanya tena kwenye maisha yangu ni kurudi nilipo toka kwani nilipoteza ramani ya maisha yangu na kwa sasa naumia kuona bado kuna vijana wanajiingiza kwenye dimbwi la utumiaji wa dawa za kulevya, vijana amkeni hakuna faida yoyote uko ila mnapoteza ramani za maisha,” alisema Hawa.

Mrembo huyo alipitia changamoto nyingi wakati alipokuwa anatumia dawa za kulevya hadi kufikia hatua ya kupata maradhi ya kuvimba tumbo kiasi cha kupelekwa nchini India kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,538FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles