23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Harmonize amtoa mke wake mitandaoni

Jessca Nangawe

STAA wa Bongo fleva, Rajab Abdul maarufu kwa jina la ‘Harmonize’ amefunguka kuwa kwa sasa hataki mke wake Sarah ajihusishe na mitandao ya kijamii zaidi kwa kuwa anamtengeneza kuwa mke wa mfano.

Harmonize ambaye alifunga ndoa na mrembo huyo raia wa Italia mwaka jana, alisema pamoja na mke wake kuwa mtu wa kujichanganya sana lakini anataka kumuona ni mtu anayejiweka karibu zaidi na familia kuliko mitandao ya kijamii na mambo mengine.

“Sitokuwa naye karibu sana kwenye shoo zangu tofauti na zamani, lakini si kwamba hamtaniona naye, nataka awe malkia, sitaki awe na mazoea na vyombo vya habari ama na watu wengine, nataka atumie muda mwingi kunijali mimi na familia yangu,”alisema Harmonize.

Alisema pamoja na kutamani mke wake awe wa kitofauti lakini hawezi kumkataza kutumia muda wake kufanya mambo ya kimaendeleo kwa lengo la kujiongezea kipato kwa kuwa ni mtu wa kujituma sana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles