24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, October 6, 2022

HATIMAYE MNANGAGWA ASHINDA URAIS ZIMBABWE

Harare, Zimbabwe


Tume ya Uchaguzi nchini Zimbabwe, imemtangaza Rais Emmerson Mnangagwa kushinda uchaguzi wa urais dhidi ya mpinzani wake Nelson Chamisa.

Matokeo ya tume hiyo yanaonyesha katika majimbo 10 yaliyotangazwa, Mnangagwa ameshinda kwa asilimia 50.8 ya kura huku mpinzani wake Nelson Chamisa, akipata asilimia 44.3.

Chamisa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha MDC Alliance, amesema kuhesabiwa kwa kura hizo hakukufanyiwa uhakiki.

Polisi waliwaondoa upinzani wakati wa kutangazwa matokeo baada ya kukataa kuyakubali matokeo hayo.

Matokeo hayo asilimia 50.8, yamemfanya Mnangagwa asiende kwenye uchaguzi wa marudio dhidi ya mpinzani wake Chamisa.

Baada ya Rais Mnangagwa kutangazwa mshindi wa kiti cha urais na tume ya uchaguzi nchini Zimbabwe ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa huu ni mwanzo mpya.

Wakati Chamisa akisisitiza kuwa ZANU-PF haikushinda uchaguzi huu, wanajaribu tu kupitisha suala lisilo na ukweli na MDC Alliance watapambana na suala hilo.

Uchaguzi huu wa Zimbabwe ni wa kwanza tangu kiongozi wa muda mrefu  Robert  Mugabe kuenguliwa madarakani.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,859FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles