22.2 C
Dar es Salaam
Thursday, September 29, 2022

EU YAKOSOA, AU YASIFIA UCHAGUZI ZIMBABWE


Baada ya Tume ya Uchaguzi nchini Zimbabwe kutangaza matokeo ya uchaguzi mkuu wa nchini hiyo na Rais Emerson Mnangagwa kushinda kiti cha urais, Umoja wa nchi za Ulaya (EU) umekosoa vikali kuchelewa kutangazwa kwa matokeo hayo.

EU wamesema kuwa waligundua baadhi ya matatizo, ikiwamo upendeleo wa vyombo vya habari, vitisho kwa wapiga kura na kutokuwa na imani na tume ya uchaguzi, vile vile mazingira ya uchaguzi hayakuboreshwa na hivyo kusababisha kuwepo kwa hali ya kiwango kikubwa cha ukosefu wa uaminifu.

Hii ni mara ya kwanza baada ya miaka 16 kwa serikali ya Zimbabwe kuwaruhusu waangalizi wa uchaguzi kutoka Muungano wa Ulaya na Marekani kuchunguza uchaguzi

Kwa upande wa Muungano wa Afrika, mapema wiki hii umesema kuwa uchagauzi huo ulikuwa huru na wa haki , akiongezea kuwa unaadhimisha wakati muhimu wa mabadiliko ya kisiasa.

Ripoti ya awali kutoka waangalizi wa SADC inasema kuwa uchaguzi huo ulikuwa wa amani na ulifanyika kulingana na sheria.

Mwakilishi wake, waziri wa masuala ya kigeni nchini Angola Manuel Domingos Augusto ameutaja uchaguzi huo kuwa kidemokrasia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,204FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles