22.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

Harry Kane auaga ukapela

LONDON, ENGLAND

NAHODHA wa timu ya taifa England, Harry Kane, ameuaga ukapela baada ya kufunga ndoa na mpenzi wake Katie Goodland baada ya kuwa kwenye uhusiano tangu wakiwa wadogo.

Taarifa za wawili hao kuwa kwenye mipango ya kufunga ndoa zilianza kusambaa mapema mwezi huu, laini wawili hao hawakutana kuweka wazi siku na sehemu ya kufanyia sherehe hiyo.

Hata hivyo walianza kwa kuposti picha zao ambazo wamevaa nguo za harusi, lakini walikuwa bado hawajafunga ndoa.

Lakini mapema jana mchezaji huyo ambaye anakipiga katika klabu ya Tottenham, aliamua kutumia ukurasa wake wa Instagram kuthibitisha kwa mashabiki zake kuwa tayari amefunga ndoa.

“Hatimaye nimefunga ndoa na rafiki yangu wa karibu, nakupenda sana Katie Goodland,” aliandika mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25.

Mbali na kuwa kwenye uhusiano kwa muda mrefu, lakini Kane alimvisha pete ya uchumba mrembo huyo Julai 2017 walipokuwa mapumzikoni huko Barbados.

Wana ndoa hao tayari wamefanikiwa kuwa na watoto wawili Ivy Jane Kane pamoja na Vivienne Jane Kane ambaye alizaliwa Agosti mwaka jana.

Baada ya Kane kuthibitisha kufungwa kwa ndoa hiyo, wachezaji mbalimbali ambao anacheza naye katika kikosi cha timu ya taifa na klabu ya Tottenham, walionesha kufurahishwa na jambo hilo na kisha kumtakia maisha mema ya ndoa.

Inaonekana wachezaji wengi hawakupewa mwaliko, lakini walitumia kurasa zao za mitandao ya kijamii kumpongeza kwa hatua hiyo muhimu katika maisha ya binadamu.

“Hongera sana Kane, umefungua ukurasa mwingine wa maisha, nawatakia kila la heri wewe na mke wako katika maisha mapya nay awe na upendo wa hali ya juu,” alisema John Terry.

Mastaa wengine ambao walimpongeza kwa kufunga ndoa ni pamoja na nyota wa mchezo wa Gofu, Rory McIlroy, nyota wa zamani wa Liverpool na Tottenham, Jamie Redknapp, mshambuliaji wa zamani wa Tottenham, Robbie Keane na wengine wengi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles